Tangazo

February 5, 2013

Matukio mbalimbali ya Moto ulioteketeza Maduka - Mwenge Bus Stand Dar

Sehemu ya mali za wafanyabiashara zilizookolewa katika maduka.

Moto mkubwa ukiteketeza sehemu ya maduka yaliyopo katika Kituo cha Mabasi cha Mwenge jijini Dar es Salaam jana. Hakuna mtu aliyepoteza maisha wala aliyejeruhiwa katika tukio hilo ambalo chanzo cha moto huo inasemekana ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika moja ya maduka hayo. PICHA ZOTE: JOHN BADI



Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakijaribu kuuzima moto huo.

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mabatini Kijitonyama, SP Edith Kiango akipata maelezo toka kwa mmoja wa wafanyabiashara mara baada ya kuwasili katika eneo la tukio.

SP Edith Kiango  akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio.

No comments: