Tangazo

February 19, 2013

TAARIFA YA MSIBA WA GRACE CHAO


FAMILIA  ya Marehemu Mathew Ndesamburo Chao wa Mazimbu Morogoro, inasikitika kuwatangazia Msiba wa Binti yao Mpendwa Grace Chao kilichotokea leo asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa Matibabu.

Mipango ya Mazishi kwa sasa inafanyika nyumbani kwa dada wa Marehemu Yopmbo kwa Abiola jijini Dar es Salaam na Maiti itasafirishwa kesho Jumaane kwenda Mazimbu Morogo na kutolewa heshima kwa ndugu jamaa na marafiki waishio Morogoro Mjini na Mzumbe.

Jumatano Mwili wa Mpendwa wetu Grace Chao, utasafirishwa kutoka Mazimbu Morogoro kwenda Marangu Mamba kwa Makundi kwa mazishi.

Mwana Mzumbe na Morogoro kwa Ujumla tunaombwa sana kushirikiana na Familia ya Marehemu katika kipindi hiki kigumu cha Maombolezo.

Taarifa hii ni kwa Mujibu wa Kaka wa Marehemu, Edwin Chao.
            
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe.

No comments: