Tangazo

May 24, 2013

Rais Kikwete aipa tuzo PSPF

 
 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Ndugu. Adam H. Mayingu  tuzo ya kuwa Mfuko wa kwanza wa Hifadhi ya Jamii Tanzania kutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama wake.  Tuzo hiyo ilitolewa kwenye maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Mifuko ya Jamii mjini Dodoma.  Mh. Raisi alisema PSPF ni mfuko madhubuti na una fursa nyingi za kimaendeleo kwa wananchi wa Tanzaniai na unauwezo mkubwa na salama katika uwekezaji . 

Aliongezea kwa kusema sio kweli kwamba Mfuko huu uko mahututi kama ilivyozungumziwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari, bali Mfuko huu unadai wadai wake Trilioni 6 na kudai sio kufilisika tena

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akisoma kipeperushi cha nyumba za PSPF zinazokopeshwa kwa wanachama wa Mfuko huo, huku akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Mfuko huo ndugu Adam H. Mayingu akimuelezea kuhusu nyumba hizo na fursa zingine zilizopo PSPF kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na ujumbe kwa Watanzania kwamba mtu yeyote mwenye umri usiopungua miaka 18 anaweza kuwa mwanachama wa PSPF

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ndugu Adam H. Mayingu akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema J. Nchimbi kuhusu shughuli za Mfuko na fursa zilizopo kwa watanzania hususani mikopo ya nyumba na mafao ya aina mbalimbali ikiwemo fao la Ujasiliamali na Elimu.
   Mtangazaji wa TBC Amina Mollel akikabidhi fomu ya kujiunga na PSPF kwa Meneja Masoko wa Mfuko huo Bi. Costantina Martin mala baada ya kuvutiwa na kukata shauri ya kuwa mwanachama wa Mfuko wa kwa njia ya uchangiaji wa hiari
 Timu ya PSPF iliyokuwa kwenye maonyesho ya wiki ya hifadhi ya Jamii wakiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wao ndugu Adamu Mayingu katikati.  Timu hiyo inastahili pongezi kutokana na uduma bora waliyokuwa wakiitoa kwa wananchi waliokuwa wakitembelea banda hilo la PSPF pale Nyerere squire Dodoma.
Wanachama wa PSPF wakipata taarifa mbalimbali ikiwapo historia ya michango yao na taarifa za uanachama.


No comments: