Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo amesema kupitia msaada kutoka Serikali ya Sweden wa kifedha ILO iliweza kuwahusisha wasichana na wavulana katika makundi mbalimbali wenye vipato vidogo kupata uelewa wa Afya ya Uzazi kupitia Makongamano, Semina na Mafunzo mbalimbali yaliyoendeshwa na shirika hilo la kazi Duniani.
Ameongeza kuwa “tuliwasaidia kuwaunganisha na vikundi vya kuweka na kukopa ili waweze kupata mitaji midogo midogo ya kufungua biashara ndogo ndogo katika harakati za kuwafanya wajitegemee na kuepekana na vishawishi vya Ngono isiyokuwa Salama.
Bw. Musindo amesisitiza Umuhimu wa TACAIDS kuandaa makongamano kama haya ili kuwawezesha wasichana na wavulana wadogo kupata ufahamu uelewa na mafunzo ya uzazi wa Afya na jinsi ya kuelewa mabadiliko yao ya kimaumbile.
“Ni matumaini yangu mwingiliano huu wa Utamaduni wa kupambana na Ukimwi, Kinga na Uwezeshwaji wa Kiuchumi umefanyika vizuri, hasa katika kuyalenga makundi yaliyo katika mazingira magumu itasaidia kuongeza kasi ya kupunguza maambukizi mapya kama ilivyoripotiwa na ripoti ya UNAIDS mwaka 2012 Duniani kwamba maambukizi mapya yamepungua kwa Asilimia 20”. Amesema.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo kwenye Kongamano hilo.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Kijakazi Mtengwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo amesema mikakati ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi inaweza kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake, Wasichana na Wavulana wadogo.
Amesema Jamii lazima itambue kuwa juhudi zaidi zinahitajika ili nchini yetu iweze kufikia malengo ya 0.3 yaani Tanzania ambayo haina maambukizi mapya ya VVU, Ukimwi usiwe sababu ya vifo, vile vile pasipo unyanyapaa wala ukatili kwa mtu yeyote anayeishi na Virusi vya Ukimwi.
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho akizungumza na washiriki amesema Takwimu zinazonyesha Wanawake wako katika hali ya hatari ya kuambukizwa zaidi kuliko wanaume ambapo mpaka sasa ni Asilimia Sita ya Wanawake nchini huambukizwa wakati wanaume ni Asilimia 3 nchini nzima.
Dr. Mrisho alisisitiza umuhimu wa kumwezesha mwanamke kiuchumi kama ndio moja ya suluhisho la kumfanya kutokuwa tegemezi katika jamii.
“Amesema takwimu zinazonyesha katika nchi nyingi za Kiafrika umaskini unachagia sana kuenea kwa Ukimwi maana Wanaume wengi hutumia umasikini wa Wasichana au Kinadada kuwarubini kwa fedha na kufanya nao Ngono isiyosalama”.
Dr. Fatma Mrisho amepongeza juhudi za ILO na kuwataka mashirika mengine na wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi kuiga juhudi zilizofanywa na ILO za kuandaa makongamano ya kiuchumi ili kumwezesha Mwanamke na wavulana wadogo kujitambua na kuelewa jukumu lao katika mapambo ya VVU na Ukimwi nchini.
Meza Kuu: Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi Tanzania (UNAIDS) Dr. Hedia Belhadj, Mwakilishi kutoka TUCTA Bw. Hezron Kaaya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Kijakazi Mtengwa, Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo, Mkurugenzi wa Sera na Utetezi wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE) Bi. Justina Lyela.
Mwakilishi kutoka shirikisho la wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Hezron Kaaya alisisitiza mshikamano na umoja wa wafanyakazi katika mapambano ya VVU na Ukimwi sehemu za kazi.
Bw. Kaaya amesisitiza majadiliano kama hayo yasiishie kwenye makabrasha bali wayatekeleze kwa vitendo ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii.
Mkurugenzi wa Sera na Utetezi wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE) Bi. Justina Lyela akitoa nasaha zake kuhusu viwango sawa vya malipo ya mishahara kwa wafanyakazi nchini ili kuwakomboa wanawake na kipato kidogo makazini.
Sehemu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchini wa Kongamano la kuwawezesha Kiuchumi Wanawake, Wasichana na Wavulana dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi lililofanyika leo jijini Dar na kuratibiwa kwa pamoja kati ya ILO na TACAIDS.
Washiriki wa Kongamano hilo wakiangalia baadhi ya machapisho mbalimbali ya VVU na Ukimwi.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo la siku moja lililofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment