Tangazo

June 27, 2013

UNIC na TAYODEA yaendesha Semina ya kupinga matumizi na biashara ya madawa ya kulevya jijini Tanga

_DSC1238
Afisa uhusiano wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akiwasilisha ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya kwenye kongamano la vijana kuhusu madawa ya kulevya mjini Tanga.
_DSC1214
_DSC1161
Afisa habari wa kituo cha taarifa cha Umoja wa mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akikabidhi Beji ya utambulisho kwa mmoja wa vijana aliyekaa miezi sita kwenye nyumba ya mafunzo ya waathirika wa madawa ya kulevya bila kutumia madawa hayo mjini Tanga katika kituo cha Tanga Sober House.
_DSC1215
Baadhi ya vijana wakifuatilia semina ya kupinga matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya iliyoandaliwa na Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kwa kushirikiana na TAYODEA.
_DSC1215
_DSC1179
Ujumbe kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa Dar es Salaam, waandishi wa habari na watumiaji wa dawa za kulevya walioonyesha nia ya kuacha kutumia dawa hizo mjini Tanga, ambao wapo kwenye nyumba ya mafunzo ya kuwawezesha kuachana na dawa hizo (TANGA SOBER HOUSE) iliyopo Tanga. Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara ya dawa za kulevya ambayo hufanyika 26 June kila mwaka. Kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika mjini Dodoma.

No comments: