Tangazo

July 5, 2013

BancABC yakaribisha Wateja kujiunga na VISA Cash Card ambayo sio lazima uwe mteja wao katika Banda lao ndani ya Viwanja vya Sabasaba

IMG_9016
Baadhi ya wafanyakazi wa BancABC wakisajili wateja wapya wa huduma ya VISA Cash Card ni Kadi ya malipo ya kabla ambayo hupunguza usumbufu wa kubeba fedha usio salama. Ambapo Mteja kuwa na kadi hii si lazima uwe na akaunti ya BancABC.
IMG_9032  
Afisa Mahusiano wa BancABC Sarah Pima akitoa maeleozo ya namna ya kutumia VISA Cash Card kwa mmoja wa wateja aliyetembelea banda la Bank hiyo lililopo karibu na Banda la Home Shopping Centre katika maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Wa pili kulia ni Afisa Mahusiano wa Bank hiyo Shamsa Aboud.
IMG_9038
Wananchi wakiendelea kupatiwa huduma na wafanyakazi wa Bank hiyo.
IMG_9045
Muonekano wa Banda la BancABC katika maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
IMG_9050
Moja ya Bango la Benki hiyo lililopo uwanjani hapo.

Zijue faida za VISA Cash Card kama ifuatavyo:-

- Una saa 24 siku 7 za juma kupata huduma kwenye akaunti yako popote, zaidi ya ATM 400 zenye nembo ya VISA ndani ya Tanzania na zaidi ya ATM milioni 1.3 duniani kote.

-Unaweza kufanya manunuzi kwenye sehemu za biashara zaidi ya 1000 zinazokubali VISA Tanzania na sehemu za biashara zaidi ya milioni 35 duniani.
-Rahisi kuipata.
-Inaweza kutumika papo hapo.
-Kuweka fedha na kuzitumia papo hapo.
-Rahisi kuweka fedha na kuzitumia haraka.
-Manunuzi ya moja kwa moja kupitia mtandao.
-Hudhibiti matumizi yako(unatumia ulichonacho kwenye kadi).
- Faraja na Usalama kupitia CHIP na namba za siri(PIN) hudhibiti udanganyifu na matumizi ya ulaghai.

-Fedha hurudishwa na kupata kadi nyingine pindi inapopotea/kuibiwa.
Ni nani anayeweza kutumia BancABC VISA Casha Card?
-Wateja na wasiokuwa wateja wa BancABC.
-Makampuni- kwa malipo ya posho na mishahara.
-Wazazi-fedha ya kujikimu kwa wanafunzi/gharama za maisha. Bora zaidi kwa usalama wa fedha.
-Mashirika ya Pensheni na Makampuni ya Bima- kwa malipo yenye faida.
-Wafanyabiashara ya Utalii- kwa malipo ya ada Utalii wa mbuga.
-Serikali- kwa malipo ya ruzuku na mikopo.
Na Unawezaje kupata BancABC VISA Cash Card?

Tembelea moja ya matawi yao ili uweze kujaza fomu fupi ya maombi ukiwa na viambatanishi vifuatavyo:

Raia- Kitambulisho cha Kura/Leseni ya Udereva/ Passport.
Sio Raia- Passport na Kibali cha makazi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nao kwa namba zifuatazo:
Upanga-Simu 255 22 2121537, 2121538, 2121539.
Kariakoo-Simu 255 22 2180212, 2180182, 2180108.
Quality Centre- Simu 255 22 2865904-910.
Arusha- Simu 255 27 2546390.

No comments: