Tangazo

July 10, 2013

DAWASCO YAJA NA MITA ZA MALIPO KADRI UNAVYOTUMIA MAJI 'LUKU'.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), Jackson Midala na Afisa Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel, Jane Matinde wakionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mita mpya za malipo ya maji kadri unavyotumia (LUKU) ambazo wateja wa shirika hilo watafungiwa. Mita hizo zimezinduliwa jana Jijini Dar es Salaam ambapo wateja wa Dawasco pia wanaweza kulipia kupitia AirtelMoney.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), Jackson Midala akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mita mpya za malipo ya maji kadri unavyotumia (LUKU) ambazo wateja wa shirika hilo watafungiwa. Mita hizo zimezinduliwa jana Jijini Dar es Salaam.

No comments: