Tangazo

July 21, 2013

Dk. Bilal: Wekezeni kutumia rasilimali za Mkoa wa Tabora

 NA JENNIFER CHAMILA  NA MAGRETH KINABO - MAELEZO

MAKAMU wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed  Gharib Bilal (pichani), amewataka wawekezaji  wa ndani na nje ya nchi kuweza katika mkoa wa Tabora kwa kutumia rasilimali zilizopo katika  sekta   mbalimbali  mkoani  humo.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Makamu wa Rais Dk. Bilal wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji la Mkoa wa Tabora liliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dares Salaam,ambalo limehusisha wadau mbalimbali wakiwemo wawekezaji, wadau wa maendeleo, wakuu wa wilaya   na wabunge wa mkoa huo.

Makamu   wa Rais , Dk. Bilal  aliwataka  wawekezaji hao  kuwekeza kwa kutumia rasilimali  ambazo ni   asali, madini,maeneo ya kihistoria, ujenzi wa hoteli,sehemu za kupumzika, viwanja vya michezo gofu, usafiri nchi kavu na angani,ufugaji wa wanyama wa porini,kampuni za kitalii, uwindaji wa wanyama, vivutio vya kiutalii vya  kiutamaduni na kihistoria.

“Serikali inawahamasisha wawekezaji wa sekta binafsi na wawekezaji ambao watashirikiana na Serikali katika maeneo hayo,” alisema Dk. Bilal.

 Dk. Aliongeza kuwa  milango iko wazi kwa uwekezaji wa miundombuni ambayo,  barabara kubwa, madaraja, mwasiliano ya simu, viwanja vya ndege, usambazaji miundombinu ya  maji, hivyo wawekezaji kutoka nje ya nchi wanaruhusiwa kuwa umiliki wa zaidi ya asilimia 100 mipango ya kuhamisha na ujenzi inaruhusiwa kupitia maeneo hayo.

Akizungumzia kuhusu suala hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Fatma Mwassa alisema wahahitaji shirikiano wa uwekezaji huo na kukuza masoko na tayari wameshaandaa mazingira mazuri.

“Ardhi tunayo tumeshaipima,tunahitaji wawekezaji katika kilimo, mafuta , nyama, maziwa na madini,” alisema Fatma.

Naye Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta alisema  mkoa huo umepata kiongozi mzuri na watendaji na umejipanga ipasavyo juu ya jambo hilo.

“Kuanzia sasa mtumishi anapimwa kwa matokeo ya kazi yake . Tusiwe  tunalalamika sisi ni masikini tutumie fursa zilizopo ili kuondoa umaskini kinachotakiwa ni uongozi usimamizi bora ili kuondokana na umaskini,” alisema Waziri Sitta.

 Mkurugenzi Mtendaji  wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC), Julieth Kairuki alisema  taasisi hiyo imejipanga vizuri ili kusaidia uwekezaji katika mkoa huo na itaweka vituo mbalimbali.

Aliongeza kuwa hivi sasa kunawawekezaji 36 waliojitokeza kuwekeza kabla ya kongamano hilo.

No comments: