Tangazo

July 22, 2013

IGP MWEMA AZINDUA UPANUZI WA ZAHANATI YA POLISI ZANZIBAR

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akipokea zawadi ya picha iliyochorwa picha yake kutoka kwa mwakilishi wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha shehia ya Mkele, Maalim Rashidi wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana. Picha zote na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

Nassir Hassan wa kikundi cha Kung Fu cha Shehia ya Nyerere akifanya onyesho la kung fu jana Visiwani Zanzibar wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akipokea zawadi ya matunda aina ya shokshok  kutoka kwa mwakilishi wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha shehia ya Ubago, Asha Suba  wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana.

Wanafunzi wa kikundi cha sanaa cha Shule ya Msingi Matopeni Unguja, wakiimba nyimbo ya kuhimiza vijana kuacha dawa za kulevya, baada ya IGP Saidi Mwema kufanya uzinduzi wa  upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani, Visiwani Zanzibar  jana.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema akipokea zawadi ya mfano wa mashua kutoka kwa mwakilishi wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha shehia ya Stone Town, Saidi Mkweche wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana.

Hapsa Omar wa kikundi cha Kung Fu cha Shehia ya Nyerere akifanya onyesho la kung fu dhidi ya mpinzani wake Nassir Hassan jana Visiwani Zanzibar baada ya IGP Saidi Mwema kufanya  uzinduzi wa upanuzi wa zahanati ya Polisi, Ziwani Visiwani Zanzibar  jana.

Hapsa Omar(kulia) na Habiba Nassor  wa kikundi cha Kung Fu cha Shehia ya Nyerere wakifanya onyesho la kung fu.

No comments: