**********************************
• NHC yathibitisha Nyumba hizo kukamilika punde• Mshindi wa kwanza kupatikana mwishoni mwa mwezi huu.
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), limewathibitishia watanzania kwamba tayari nyumba tatu zinazoshindaniwa katika promosheni ya Airtel Yatosha zimekamilika na tayari mafundi wanafanya matengenezo ya mwisho tayari kwa kukabidhiwa kwa washindi hao.
Meneja Mawasiliano wa NHC, Yahaya Charahani alibainisha hayo mwishoni mwa wiki wakati wanahabari kutoka vyombo mbali mbali walipotembelea nyumba hizo kujionea jinsi mradi huo uliopo Kibada karibu kabisa na Tuangoma wilayani Temeke unavyokwenda.
“Nyumba hizi tatu zenye vyumba vitatu vya kulala, jiko, sebule nzuri pamoja na sehemu ya nje iliyonakishiwa kwa umakini ili kuipa nyumba mvuto wa hali ya juu zimejengwa kwa gharama ya milioni 194/- tayari zimekamilika na pindi washindi watakapotangazwa wataweza kuhamia katika nyumba hizi mara moja tu." alisema Charahani.
Aidha aliwataka wateja wa kampuni ya Airtel kuzitembelea nyumba hizo na kujionea wenyewe kiwango cha ubora wa nyumba hizo, ili waweze kuhamasika zaidi kushiriki katika promosheni hiyo.
Nae Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando aliwataka Watanzania kuendelea kutumia mtandao wa Airtel hususani huduma ya Yatosha kwa kupiga *149*99# na kuchagua vifurushi vinavyowatosha ili kujihakikishia nafasi ya kushinda nyumba hizo.
"Airtel imedhamiria kutatua matatizo ya wateja wake kwa kutoa huduma nafuu na bora kuliko mtandao wowote lakini pia promosheni hii ya YATOSHA inalenga kubadilisha maisha ya Watanzania hasa wale wanaotumia mtandao wetu wa Airtel." alisema Mmbando.
Alifafanua kuwa katika promosheni hiyo jumla ya million 284/- zitatumika kuwazawadia wateja wa kampuni hiyo, ambapo milioni 194/- zitanunua nymba hizo tatu kutoka NHC na kiasi kinachobaki kwa siku 90 Airtel itatoa milioni moja kwa mshindi mmoja kila siku.
No comments:
Post a Comment