Video na Joshua Mmali
Oliver Mtukudzi alitoa burudani bure kwa wakazi wa New York katika eneo la kupumzika Free Park, maelfu ya wamarekani walifurika katika show yake. Hii inafundisha nini wasanii wa nyumbani Tanzania? Nafikiri kuna jambo kubwa sana la kujifunza toka kwa mkongwe huyu.
Oliver si mjinga kutoa burudani ya bure, wasanii wetu toka Tanzania inabidi waige mfano huu ili mziki wao uanze kuwaingia wamarekani na hata mataifa mengine ya nje. Nazungumzia msanii kujulikana na kukubalika katika kiwango cha kimataifa katika soko la mziki la dunia.
Namalizia kwa kuwapongeza mapromota wote wanaowatafutia show wasanii toka nyumbani kutoa burudani nje ya nchi. Kwa kweli wanafanya kazi nzuri. Sasa nawaomba waanze kutafuta masoko nje ya jamii zetu za kitanzania na Afrika mashariki kwa ujumla. Hii namaanisha sio kuimba pekee katika klabu za wabongo ama wakenya. Mtakubaliana nami wasanii mliowahi kutoka nje ya Tanzania nadhani mnaelewa nachosema. Sisi mashabiki wenu tunataka kuona mkipanda na kushiriki katika majukwaa makubwa yanayoheshimika duniani. Ni furaha yangu nitakapoona msanii wetu anatoa burudani katika viwanja vikubwa hapa Marekani na kwingineko, naamini inawezekana.
kuona mengi toka Swahili TV Mtaani Kunani tembelea www.swahilitv.blogspot.com
No comments:
Post a Comment