Tangazo

Showing posts with label Kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Kimataifa. Show all posts

March 26, 2018

DJ Luke Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV 2018

Matokeo ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Lucas Mukami (DJ Luke) ibuka mshindi wa Urais wa Jumuiya ya Watanzania DMV kwa kura 315, dhidi ya Liberatus Mwang'ombe, aliepata kura 262. akifuatiwa na Rebeca 24.

VICE PRESIDENT Joha 352 Joyce 248. SECRETARY Cleopatra 311 Omby 214 Dotto 70. ASST SECRETARY Saria 360 DMK 23. ASST. TREASURY Magret 263 Mikidadi 329.... BOARD Mashaka 413 Zena 296 Jabil 330. Pius 454 Asha 386 Hamza 295 Ruth 250.

March 6, 2018

Mdahalo wakuwania Uongozi wa Urais Jumuiya ya Watanzania DMV

Huu ni Mdahalo wa Sehemu ya kwanza kati ya mbili zijazo, wa kugombania kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Urais kupitia Jumuiya ya Watanzania waishio DMV, ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi, Siku ya Jumamosi March 3, 2018 katika ukumbi wa Indiana Springs Terrance Local Park Sliver Spring Maryland Nchini Marekani.

February 12, 2018

UNESCO KUADHIMISHA SIKU YA RADIO DUNIANI DODOMA

Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania (TADIO) wataaungana na Dunia nzima kuadhimisha Siku ya Redio Duniani. Maadhimisho hayo yatafanyika Dodoma mnamo Tarehe 13/ Februari mwaka 2018 na yatajumuisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani na Wadau wengine wa habari. 

  Kauli Mbiu ya Redio Jamii mwaka 2018 ni Redio na Michezo huku msisitizo mkubwa ukielekezwa kwenye utandawazi katika suala la kutoa kipaumbele cha kutangaza michezo, usawa wa kijinsia katika michezo na kutangaza michezo pamoja na kuhuisha amani kupitia michezo. 

  Maadhimisho hayo yatajumuisha maada juu ya kauli mbinu na miiko ya uandishi wa habari mtandaoni, Kanuni za Mtandaoni za mwaka 2017 pamoja na kuchagizwa na mdahalo juu ya michezo. 

  Mgeni Rasmi katika maadhimisho haya atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe. 

  Mnamo January 14, 2013, Umoja wa Mataifa uliidhinisha rasmi Tamko la UNESCO katika Mkutano wake Mkuu wa 67 juu ya Siku ya Redio Duniani. Azimio hilo lilipitishwa katika kikao cha 36 cha UNESCO na kutamka kuwa February 13 itakuwa siku ya Umoja wa Mataifa ya Redio. 

  Mpaka sasa, Redio imeendelea kuwa chombo cha uhakika huku kikibadilika kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kutoa mbinu mpya kwa jamii kuwasiliana na kushiriki. Redio ina nafasi kubwa ya kuzileta jamii pamoja na kuhuisha majadiliano ya kuleta mabadiliko chanya. Kwa kusikiliza halaiki, na kujibu mahitaji yao, radio inatoa wigo wa Maoni na sauti zinazohitajika kutatua changamoto katika nyakati hizi. Radio ni, na inaendelea kuwa njia yenye nguvu katika nchi zilizo Nyingi za bara la Afrika. 

 Si tu redio inatumika kubadilishana Taarifa katika jamii bali pia ni nafuu na inafikika. Maadhimisho haya yametanguliwa na mafunzo ya siku saba kwa waandishi wa habari wa redio jamii juu ya uhariri, kuandaa vipindi na kufanya ufuatiliaji wa masuala mtambuka katika jamii. 

  Mafunzo hayo yamejumuisha waandishi 49 kutoka vyombo vya habari vya kijamii kutoka redio 24 zinazofadhiliwa na UNESCO ikiwa ni asilimia 77.4 ya mikoa yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Washiriki wa mafunzo hayo wanajumuisha Waandishi na Maripota pamoja na maafisa tathmini ambao awali walipata mafunzo ya tathmini na ufuatiliaji kutoka UNESCO. Shirika la UNESCO kwa msaada kutoka Shirika la SDC wanasaidia utekelezaji wa mradi unaolenga kuzijengea uwezo redio jamii katika nyanja za ushiriki katika michakato ya kidemokrasia na maendeleo. 

  Mradi huo unalenga kukuza na kujenga uwezo wa redio jamii takribani 25 nchiini Tanzania kwa kukuza nafasi yao kama watoa huduma za jamii, kupanua wigo wa kijiografia katika masuala ya habari mtambuka katika maeneo yao na kuboresha uwezo wao katika kazi.

January 26, 2018

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akutana na Sheikh Saud Bin Saqr katika Makaazi yake Nchini Ras Al Khaimah

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza Mtawala wa Ras-Al-Khaimah Mtukufu Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi na kufanya nae mazungumzo yaliolenga kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya pande mbili hizo.

Mazungumzo hayo yaliofanyika katika makaazi ya Sheikh Saud  Bin Saqr Al Qasimi mjini Ras-Al-Khaimah, ambapo viongozi hao kwa pamoja walieleza haja ya kuendeleza uhusiano na kuimarisha mashirikiano katika kuinua sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya mafuta na gesi asilia.

Aidha, viongozi hao walizungumza juu ya hatua zinazoendelea katika suala zima la utafiti wa mafuta na gesi asilia ambapo katika mazungumzo hayo walieleza haja ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa pamoja ili kufikia lengo la kuipaisha Zanzibar kiuchumi na kimaendeleo.

Katika maelezo yake, Dk. Shein alitoa shukrani kwa kiongozi huyo kutokana na juhudi zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na kumpongeza kiongozi huyo kwa mafanikio yaliopatikana nchini humo katika kipindi kifupi.

Rais Dk. Shein alimueleza kiongozi huyo kuwa Zanzibar ina mengi ya kujifunza kutoka kwa ndugu zao wa Ras Al Khaimah na iko tayari kupanua wigo wa maendeleo kutoka nchini humo kwani inatambua mafanikio yaliopatikana kutokana na mikakati iliyowekwa.

Pamoja na hayo, viongozi hao kwa pamoja walizungumzia hatua zaidi zinazohitajika katika kuimarisha ushirikiano kati ya Zanzibar na Ras Al Khaimah katika sekta za maendeleo ikiwa ni pamoja na kupanga mipango madhubuti katika malengo yaliokusudiwa ya hapo baadae.

Nae Kiongozi huyo alieleza kuwa Ras Al Khaimah itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake na Zanzibar hasa katika sekta hizo za maendeleo na kusisitiza kuwa uhusiano na ushirikiano huo utaletea maendeleo makubwa Zanzibar hasa kwa kutambua kuwa jambo hilo limo kwenye dhati ya moyo wake.

Alieleza kuwa uhusiano na ushirikiano huo wa kihistoria uliopo una malengo ya kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata maendeleo endelevu huku akizipongeza juhudi na kasi za Rais Dk. Shein za kuhakikisha Zanzibar inapiga hatua za kiuchumi.

Katika maelezo yake Mtawala wa Ras Al Khaimah alimuhakikishia Rais Dk. Shein kuwa atandelea kumuunga mkono ili kuhakikisha malengo yaliokusudiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kupambana na umasikini na kukuza uchumi yanatekelezeka kwa vitendo kwani kuna kila dalili za kuyatekeleza kutokana na juhudi anazoziona ambazo zinafanywa na Dk. Shein pamoja na Serikali anayoiongoza.

Wakati huo huo, Dk. Shein alikutana na uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia  ya Ras Al Khaimah “Rak Gas”, iliyopo mjini Ras Al Khaimah ambapo katika maelezo ya uongozi wa Kampuni hiyo walimueleza Dk. Shein hatua zilizofikiwa za utafiti wa mafuta na gesi asilia Zanzibar.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Kamal Ataya alimpongeza Dk. Shein kwa ziara yake hiyo na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo huku akisisitiza kuwa Kampuni yake itahakikisha utafiti unaofanyika unakuja na majibu mazuri.

Dk. Shein kwa upande wake alitoa pongezi zake kwa Mtawala wa Ras Al Khaimah pamoja na kuipongeza Kampuni hiyo kwa jitihada zake inazochukua katika kuhakikisha malengo yaliokusudiwa yanafikiwa na hatimae kuleta tija.

Mapema, Rais Dk. Shein akiwa na ujumbe wake akiwemo Mama Mwanamwema Shein, walitembelea eneo la Kisiwa cha Al Marjan ambacho kimetengezwa baada ya kufukiwa kwa bahari na kuwa mji wa kisasa wa kitalii na uwekezaji.

Akiwa katika eneo hilo, Dk. Shein alipata maelezo juu ya hatua zilizochukuliwa katika kulitengeneza eneo hilo la bahari na sasa kuwa ardhi iliyojengwa hoteli za kisasa ambazo zimekuwa ni kivutio kikubwa cha watalii kutoka sehemu mbali mbali duniani.

Aidha, uongozi wa Kisiwa hicho ulimueleza Rais Dk. Shein hatua zilizochukuliwa katika kuhakikisha hata watalii wakiwemo wananchi wa Ras Al Khaimah wanapata fursa ya kutalii katika eneo hilo kwa kuweka viwango vya chini vya malipo ya hoteli hizo  ili kuhakikisha wenye vipato vya chini nao wanafaidika.

Dk. Shein akiwa nchini Dubai pia, alipata fursa ya kukutana na ujumbe wa Utaratibu wa Mfuko unaojulikana kwa jina la “Khalifa Fund” ambapo uongozi wa Mfuko huo ulimueleza Rais Dk. Shein namna unavyotoa fursa zake na kuahidi kutoa ushirikiano kwa Zanzibar hasa katika mpango wa kuwawezesha vijana kujikomboa na ajira na kuahidi miongoni mwa nchi zitakazowapa kipaumbele Zanzibar itakuwa ni ya mwanzo.

Rais Dk. Shein amemaliza ziara yake ya wiki moja katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na anatarajiwa kurejea nchini kesho Jumamosi, tarehe 27 Januari, 2018.
Ziara hiyo ya Dk. Shein ilianza kwa kufanya mazungumzo na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya (UAE) nchini Abu Dhabi ambapo pia,alifanya mazungumzo na  Mohamed Saif Suwaid, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Abudhabi “Abudhabi Fund for Development”, na kutembelea mji wa Nishati, Masdar, msikiti wa Shaikh Zayed pamoja na sehemu ya kihistoria ya Wahat Al Karama.
Aidha, Dk. Shein alifanya ziara nchini Dubai kufanya mazungumzo na Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid Al Makhtoum, Makamo wa Rais na Waziri Mkuu wa (UAE) na Mtawala wa Dubai, alitembelea Bandari ya Jebel Ali, alikutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wawekezaji na Wenyeviwanda wa Dubai na kutembelea Mji mpya wa kisasa wa Nakheel pamoja na Mradi wa Palm Jumeirah.
Dk. Shein alifanya ziara mjini Sharjah na kukutana pamoja na kufanya mazungumzo na Mtukufu Dk. Shaikh Sultan Mohammed Al Qasimi, Mtawala wa Sharjah,akiwa Sharjah, alitembelea eneo la shughuli za uvuvi la ‘East Fishing Processing LLC” pamoja na shamba la ngombe wa maziwa la Al Rawabi.

Pia, Dk. Shein alifanya ziara Ras Al Khaimah na kukutana pamoja na kufanya mazungumzo na Mtukufu Shaikh Saud Saqr Al Qasimi, Mtawala wa Ras Al Khaimah pamoja na kutembelea Makao Makuu ya Kampuni ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na gesi asilia  ya Ras Al Khaimah “Rak Gas” pamoja na kutembelea kisiwa cha Al Marjan.

Katika ziara hiyo, Dk. Shein alifuatana na viongozi mbali mbali akiwemo Mkewe Mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Salama Aboud Talib, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Khalid Salum Mohamed, Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum Juma Ali Khatib,pamoja na Mshauri wa Rais Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa.

Wengine ni Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Juma Ali Juma, Balozi Mohamed Haji Hamza Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa upande wa Zanzibar, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), Salum Khamis Nassor pamoja na watendaji wengine wa Serikali. 
 Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar


December 7, 2017

Ubalozi wa Norway waipatia UN Tanzania dola milioni 5.1 ili kufanikisha UNDAP II

Ubalozi wa Norway nchini umeipatia msaada wa dola bilioni 5.1 Umoja wa Mataifa Tanzania ili kusaidia kufanikisha Mpango wa Misaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II). Makubaliano hayo yamesainiwa na Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez katika ofisi za ubalozi wa Norway uliopo jijini Dar es Salaam. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi Kaarstad alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo inatolewa na Norway ili kufanikisha mpango wa UNDAP II ambapo kwasasa imefika dola milioni 10.5 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali na UN katika mpango huo.
Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa Umoja wa Mataifa Tanzania. (Picha zote na Rabi Hume)
"Lengo la msaada huu ni kuwasaidia wakimbizi waliopo Kigoma na kwa wananchi wa Kigoma kwa ujumla, makubaliano mapya tuliyosaini leo yanalenga maeneo yaliyokusudia. Kusaidia kilimo ili kuwezesha kuwepo chakula cha kutosha kwa ajili ya wakimbizi na wananchi wanaozunguka hayo maeneo ya kambi, "Sehemu nyingine ambayo msaaada huu unalenga, ni kusaidia ni kumaliza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto. Matumaini yetu msaada huu utafungua milango kwa washirika wengine wa maendeleo kuchangia ili kufanikisha mapango huu," alisema Naye Rodriguez aliushukuru Ubalozi wa Norway kwa msaada waliowapatia na kwa serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao inautoa kwa Umoja wa Mataifa ili kufanikisha mpango huo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez akizungumza kuhusu msaada ambao wameupokea kutoka Ubalozi wa Norway.
Rodgriguez alisema msaada huo utatumika kama ulivyopangwa kwa wakimbizi na wananchi waliopo mkoa wa Kigoma kwa kuhakikisha kunakuwa na chakula cha kutosha kwa wakimbizi wote wanaokadiriwa kufikia 340,000, lakini pia kuhakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia kwa watu wote. "Kwa miongo mingi, Norway imeendelea kuwa mshirika wa kuaminika kwa Tanzania na Umoja wa mataifa. Kwa kuweka mkazo katika mahitaji ya wanawake na watoto walio hatarini, rasilimali hizi zitatoa mchango muhimu katika kukidhi mahitaji ya wenye uhitaji mkubwa kama ilivyoelezwa katika Malengo ya Dunia." alisema Rodriguez.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez na Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marrie Kaarstad wakisaini makubaliano ambayo yatawezesha Norway kuongeza dola milioni 5.1 katika makubaliano ya Mpango wa Misaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II).

September 27, 2017

Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO katika Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari Sept 28

Katika ulimwengu wa uchangamano, ufikivu wa habari ni muhimu katika kujenga jamii yenye maarifa, iliyo shirikishi na endelevu. Huu ndio ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote (IDUAI), ukizingatia jukumu muhimu ambalo ufukivu wa habari hufanya katika kuendeleza Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu. Ufikivu habari ni haki ya msingi. Inawawezesha wanawake na wanaume kuelewa na kushiriki katika kujenga na kushirikiana ujuzi wanaohitaji ili watoe mchango kikamilifu katika jamii yao. Raia wenye taarifa sahihi huifanya serikali iwajibike. 

Ufikivu Habari ni dereva wa uvumbuzi na ubunifu, kuongeza fursa kwa wote, hasa kwa wasichana na wanawake. Ufikivu habari huanza na kujitolea kwa Serikali kutengeneza, kueneza na kutekeleza sera na sheria zinazohusu haki ya habari na kuhakikisha kuheshimiwa kwa haki hii ya kibinadamu. Hii inahitaji utaratibu wa ufanisi wa utekelezaji na utamaduni wa uwazi katika aina zote za taasisi. Wananchi wanahitaji pia kuwa na fikra pana, ujuzi wa kusoma na ujuzi wa kidigitali ambao unahitajika kufikia, kuchambua na kutumia habari kwa njia tofauti, nje na ndani ya mitandao. 

Hii ndiyo maana UNESCO inaziomba serikali zote na washirika kutumia uwezo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kusaidia kufikia Lengo la 4, Elimu Endelevu inayolenga kuhakikisha "elimu shirikishi, sawa na ya ubora na kukuza fursa za elimu isiyo na mwisho kwa wote; Ufikivu wa Habari pia unajumuisha kukuza uandaaji wa maudhui yanayofaa, yenye kulenga jamii husika na yanayopatikana kwa lugha mbalimbali. Yote hii inahitaji sera zenye ufanisi na ushirikiano mzuri katika ngazi zote. Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote pia ni fursa ya kurejea ahadi yetu ya uhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa habari. Vyombo vya habari huchukua nafasi muhimu katika kuwezesha ufikivu wa habari kwa wananchi na katika kufuatilia masuala muhimu ya kijamii na wakati huo huo vikiwaelimisha wafuatiliaji kwa kuwapa ufahamu na ujuzi. Haiwezekani kuwepo kwa ufikivu wa habari kwa wote bila kuwepo kwa vyombo vya habari vilivyo huru. Ufikivu wa habari sio tu ni lengo peke yake; pia ni mchangiaji muhimu katika utekelezaji wa malengo mengine yote ya Maendeleo Endelevu. Kwa hiyo ni muhimu tuendeleze juhudi zetu ili kuhakikisha kuwa kila mwanamke na mwanamume wanafurahia ufikivu kamili wa habari.

September 21, 2017

SALAMU ZA MKURUGENZI MKUU WA UNESCO SIKU YA KIMATAIFA YA AMANI

Pamoja kwa ajili ya Amani: Heshima, Usalama na Utu kwa Wote 

  Hii Siku ya Kimataifa ya Amani huadhimisha nguvu ya ushirikiano wa kimataifa katika kujenga ulimwengu wa amani na endelevu. Jambo hili linazidi kuwa ni la muhimu sana hasa wakati huu tunapokumbana na changamoto zisizo za kawaida. Nguvu mpya za mgawanyiko zimeibuka, zikieneza chuki na kuondoa kuvumiliana. 

Ugaidi unachochea vurugu, wakati misimamo mikali inapandikiza sumu ndani ya fikra dhaifu za vijana. Katika maeneo maskini zaidi ya dunia na yasiyo na maendeleo, majanga ya asili yanayohusiana na hali ya hewa yanazidisha hali ya kukosa utulivu, yakiongeza idadi ya watu wanaolazimika kuhama makazi yao na kuongeza zaidi hatari ya kutokea kwa vurugu. 

  Vikwazo vya kuifikia amani vina utata mwingi na ni vigumu sana - hakuna nchi moja peke yake inayoweza kuviondoa vikwazo hivyo. Jambo hili linahitaji aina mpya ya mshikamano na hatua za pamoja, na kuanza kuchukua hatua hizo mapema iwezekanavyo. 

  Hiki ndicho kilichoko katika moyo wa wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kuongeza jitihada zinazolenga kuendeleza amani, kuzishirikisha Serikali na mashirika ya kiraia, pamoja na jumuia za kimataifa na za kikanda. 

  Mabadiliko yanaenea duniani kote kwa kasi kubwa – ni lazima lengo letu liwe kuyapokea mabadiliko hao katika misingi ya haki za binadamu, kuyapa mwelekeo chanya utakaotupeleka kwenye dunia iliyo ya haki zaidi, jumuishi zaidi na endelevu zaidi. 

  Utamaduni wa amani ni utamaduni wa mazungumzo na kuzuia uvunjifu wa amani, na katika muktadha huu, jukumu la Umoja wa Mataifa halijawahi kuwa la muhimu sana kama wakati huu. 

Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu inathibitisha kwamba "hawezi kuwa na maendeleo endelevu bila amani na hakuna amani bila maendeleo endelevu". Moyo huo huo unaungwa mkono na maazimio ya Umoja wa Mataifa kupitia Baraza la Usalama na Mkutano Mkuu ya mwaka 2016 yanayohusu “amani endelevu”.

Tunahitaji namna mpya yenye kina zaidi, itakayoshughulikia sababu za msingi, na kuimarisha utawala wa sheria na kukuza maendeleo endelevu, yote haya katika misingi ya majadiliano na kuheshimiana. Hii ndiyo dira ya hatua zote za UNESCO za kujenga amani kupitia elimu, uhuru wa kujieleza, majadiliano kati ya tamaduni mbalimbali, heshima kwa haki za binadamu na kutambua uwepo wa tamaduni mbalimbali na ushirikiano wa kisayansi. 

  Katika hii Siku ya Kimataifa ya Amani, imetupasa wote tuweke upya ahadi na nia zetu za kujenga umoja wa kimataifa. Ili kuendeleza amani, ni lazima tuijenge amani kila siku, katika kila jamii, na kila mwanamke na mwanaume, kwa kufanya kazi pamoja ili kufikia wakati ujao ulio bora zaidi kwa wote.

August 24, 2017

JANUARY MAKAMBA AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA DIASPORA ZANZIBAR

Na Mathias Canal, Zanzibar

Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) limefunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 kwa kuwashirikisha washiriki wapatao 350, ambapo miongoni mwao wanadiaspora wamehudhuria zaidi ya 200 na watendaji kutoka taasisi za Serikali zote mbili wakiwa ni 150.

Diaspora wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini katika sekta ya kuimarisha na kuanzisha viwanda ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB)  alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi litakalodumu kwa siku mbili Agosti 23 na 24, 2017 katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel uliopo katika kijiji cha Kama Wilaya ya Magharibi A.

Mhe Makamba alisema kuwa kwa sasa Demokrasia imeimarika nchini kutokana na serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kukubaliana kwa kauli moja kuimarisha usalama wa wananchi ili kurahisisha uimara wa uwajibikaji wa ujenzi wa Taifa.

Alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa kuna changamoto nyingi zinazowakabili Diaspora ikiwemo ucheleweshwaji wa uwekezaji sambamba na kutokuwepo sera ya utambuzi dhidi yao lakini changamoto hizo zinaendelea kutatuliwa na hatimaye kumalizika kabisa.

Changamoto zingine ilikuwa ni pamoja na kuwepo kwa uraia wa nchi mbili ambapo Mhe Makamba alisema kuwa serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwani halipo katika uhalisia kwa sasa kwa kutokuwepo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze kutumia fursa ya uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia fursa muhimu za uwekezaji katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa Diaspora wenyewe, watanzania waishio nchini na Taifa kwa ujumla wake.

Alisema kuwa Diaspora ni kiungo muhimu katika kuchangia sehemu kubwa ya maendeleo endelevu katika nchi zao za asili kwa kuchangia katika uhamishaji wa rasilimali, ujuzi na mawazo na hatimaye kupelekea nchi yao kunufaika na uchumi wa kidunia unaoonekana kukua siku hadi siku.

Alisema kuwa fedha zinazotumiwa na Diaspora katika nchi wanazoishi ni miongoni mwa vyanzo vinavyosababisha ukuaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, fedha hizo zitakapotumika vizuri kwa uwekezaji katika biashara na vitega uchumi ndio huwa chanzo na kichocheo cha ukuaji jadidifu wa pato na uchumi wa nchi zinazopokea fedha hizo.

Aidha, Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeweka msisitizo na juhudi za kukusanya mapato ili kukuza uchumi wa Tanzania na uwezo wa serikali kujiendesha.
Mhe Mkamba aliwasihi Diaspora kufuata kanuni,taratibu na sheria katika nchi wanazoishi ili kuendelea kuiweka Tanzania katika sifa nzuri ya kuwa na wananchi wenye kufuata sheria na taratibu.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeratibu Kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) kwa minajili ya kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano hilo ni mwendelezo wa makongamano matatu ya awali yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 Jijini Dar es Salam na mwaka 2016 lililofanyika Mjini Zanzibar.

Lengo kuu la makongamano hayo ni kwa Serikali na wanadiaspora kukutana, kubadilishana mawazo na kuwashajihisha wanadiaspora kuwekeza nchini kwao kwa maslahi yao na kwa ustawi wa uchumi wa taifa lao.

Kongamano hili la nne la Diaspora limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”

Katika hatua nyingine washiriki wote wamepata fursa ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuboresha umoja huo wa watanzania waishio nje ya nchi sambamba na kutoa maoni yao kwa serikali kwa dhamira ya kuwa na Umoja na ushirikiano bora kati yao na serikali.

Pia walitembelea shamba la BIG BODY SPICE linalolima mazao mbalimbali ya
viungo ikiwemo mazao ya Pilipilimanga, Mdalasini, Kahawa, Hiliki, Vanila,
Mdoriani, Kakao, Karafuu, Tangawizi, Mrangirangi na Mkungumanga.
 
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibarBaadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Ndg Geofrey Mwambe akizungumza wakati wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni linalofanyika Sea Cleaf Hotel Mjini Zanzibar
Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo

Dkt Hamed Hikmany (Katikati) akiongoza mada kuhusu Ushauri wa uwekezaji kwa siku zijazo mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar
Mhe Hassan Khamis (Katikati) akiongoza mada kuhusu Jukumu la jumuiya ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi katika uwekezaji sambamba na Diaspora na nchi yao katika maendeleo endelevu mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar


August 12, 2017

The Commonwealth Secretary General Rt Hon Barones Patricia Scotland QC meets Zanzibar President, visits some of the Isles attractions

 The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC (left) accompanied by Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro and Ambassador Celestine MushyDirector of  Multilateral Cooperation in the Ministry of Foreign Affairs and Regional Affairs head to the plane ready to take off  for their one day trip of  Zanzibar
 The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC greets the crew before boarding
Top Zanzibar government officials receive The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia atScotland QC at the Karume International Airport in the isles
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC signs the visitor's book upon arrival at the Abeid Amani Karume International Airport. On her right is Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma and left is Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro

The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC upon arrival at the Abeid Amani Karume International Airport. On her left  is Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma and Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC arrives at the Zanzibar State House accompanies by Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein receives The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC at the State House
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein and The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC fields questions from journalists at the State House
 The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC poses for a souvernier photo with Isles based ITV and Radio One journalist Farouq Karim  at the State House
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC is taken to a tour of Stone Town with The House of Wonders in the background
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC and her entourage pose for a group photo
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC and her entourage pose for another group photo
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC and her entourage take a guided walking tour through spice plantations
During the Spice tour the Baroness  and her entourage saw how the spices, herbs and fruits are cultivated, with the  tour guide describing in detail all about them as well as tropical fruits such as cloves, lemongrass, nutmeg, cinnamon, turmeric, vanilla, coconuts, papaya, chilli, black pepper, jackfruit, cardamom, cassava and oranges.
The  tour guide describes in  detail  how the spices, herbs and fruits  can be used
Visibly happy with the tour, our visitor is
More spices and herbs are shows
Even lipstick from plants was applied 
Some of the many tourists taking the spice tour cool off the day with coconut juice under clove trees
The baroness joins in
Neatly packed spices and herbs are on display
The visitors take their leave after a satisfying spice tour
Off to the State House where a sumptious luncheon in her hnour awaits
After  the luncheon and on behalf of the entourage Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro thanks their host President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein 
Thank you, Your Excellency, for the sumptious luncheon....
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein  leads the Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC outside for souvenir photos.
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein take the first photo with the  Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC at the State House
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein and the  Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC are joined by the Zanzibar Chief Secretary Dr.  Abdulhamid Yahya Mzee (left)  Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma, Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro and Minister for Finance and Planning Dr. Khalid Salum Mohamed
The VVIPs are joined by the rest of the entourage
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein bids farewell to the  Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC
At the airport The Vice President of the United  Republic of Tanzania Hon. Samia Suluhu Hassan meets the Baroness
The Vice President of the United  Republic of Tanzania Hon. Samia Suluhu Hassan bids farewell to  the Baroness
Its time for the Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC to depart
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC is bid farewell 
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC  bids farewell to Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma

The Baroness waves goodbye...
....and blows kisses to her hosts
Salutes welcome them back to Dar es salaam
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC greets the police officers
"...What a tour"
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC caps off the day with a courtesy call on  Prof Palamagamba Kabudi,  Minister for Justice and Constitutional Affairs at his office in Dar es salaam
The Baroness greetsb Prof Sifuni Mchome, Permanent Secretary in the Ministry of Justice and Constitutional Affairs
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC  holds talks with   Prof Palamagamba Kabudi,  Minister for Justice and Constitutional Affairs at his office in Dar es salaam.