Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Dk.Meshack Shimwela alipowasili Hospitalini hapo kukabidhi msaada wa taa za chumba cha upasuaji kwenye Hospitalini hiyo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa hospitali ya Amana na wafanyakazi wake wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa taa za chumba cha upasuaji katika hospitali hiyo inayohudumia wakazi wa Manispaa ya Ilala yenye kadirio la wakazi 1,179,992sqkm ambapo pia Hospitali ya Amana hutoa huduma kwa wakazi wa Manispaa zingine na hata Mikoa ya Jirani.
Picha juu na chini Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akikabidhi rasmi msaada wa taa hizo kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Dk.Meshack Shimwela kwenye hafla fupi iliyofanyika hospitalini hapo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa akiongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Dk.Meshack Shimwela (kulia) kuelekea kukagua chumba cha upasuaji katika hopspitali hiyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa kupitia wadau wake ametoa msaada wa taa hizo zenye thamani ya shilingi Millioni sita laki saba na tisini elfu 6,790,000/= ambapo msaada huu wa taa umefika kwa wakati muafaka utakaowawezesha madaktari kuwahudumia wagonjwa wengi na kupunguza msongamano mkubwa wa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ambao kwa hakika walilazimika kufanya pasuaji muda wa mchana peke yake hali ambayo ilisababisha msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo.
Kwa upande wa huduma ya upasuaji hospitali ya Amana inahudumia wagonjwa kati ya 20 mpaka 30 kwa siku kwa kutumia theater mbili ambazo ni main theater na maternity theater zenye vyumba vinne vya upasuaji (theater rooms). Kwa muda mrefu Hospitali hiyo ilikuwa inakabiliwa na tatizo la kuharibika kwa taa ya upasuaji (operating lamp) ambayo imepelekea kutumia vyumba vitatu vilivyopo theater kubwa (Main theater).
No comments:
Post a Comment