Nyaraka ya Profesa Muhongo |
Septemba 7, 2013 nilipokea barua pepe (email) yenye
kichwa cha habari kisemacho “ubinafsi/ufisadi wa MENGI na Chuki/Fitina kwenye
Maendeleo”.
Aliyetuma email hiyo alijitambulisha kama “CCM
TANZANIA” na email ilisambazwa kwa vyombo vya habari, waandishi na watu wengine
wengi wakiwamo wanasiasa. Kabla ya hapo nilifowadiwa nakala ya ujumbe (SMS) na
watu ambao walitumiwa na Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini
na Mbunge inayosema;
|
“Ambieni Watanzania: Kampuni za Mengi zimeshikilia vitalu 59 vya
madini vyenye ukubwa wa mita za mraba 3,752.37 (sq km) Amevishikilia,
ameshindwa kuviendeleza. Watanzania wanakosa mapato na ajira! Sasa anataka
vitalu vya gesi na mafuta. Je huu ndio uzawa?|
|
|
Na
|
“Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya
raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu.”
|
|
Vile vile Septemba 5, 2013 Profesa Muhongo akijibu
swali la Mwandishi wa habari lililouliza;
|
“Mhe. Waziri tunataka ufafanuzi kuhusu kauli yako ya hivi karibuni
kwamba waTanzania hawana uwezo wa kuwekeza katika uwekezaji wa gesi asilia.
Kwanza kauli hii ni kweli? Pili kauli kwamba Watanzania wanaweza
kuwekeza kwenye sekta ya machungwa tu huoni kwamba si kwamba unawavunja moyo
bali unadhalilisha wewekezaji wazalendo?”
|
|
Na Profesa Muhongo akajibu:
|
“Kila mtu alitoa mawazo ya sera ya gesi wakiwemo TPSF. Mengi na
wenzake wanataka vitalu wafanye ulanguzi wa gesi na mafuta yetu. Tutatoa
orodha ya vitalu vya madini vilivyoko mikononi wa Mengi ambavyo anafanya
ulanguzi. Ukweli utaonyesha ubabaishaji na ulanguzi wa Mengi wa genge lake.”
|
|
Nimeona ni vyema nitumie haki yangu ya kujibu
(right of reply), lakini kwa wale wanaohusika kusambaza taarifa hizo kuchafua
jina langu wajue kwamba kujibu kwangu hakuondoi haki yangu ya kuchukua hatua za
kisheria.
Kuingizwa kwa vitalu vya madini katika hoja ya gesi
Huo ni upotoshwaji wenye lengo la kututoa kwenye
hoja ya msingi ya rasilimali yetu ya gesi. Sijawahi kufanya udalali kwenye
vitalu vya madini. Huu ni uongo wa hali ya juu.
Tamko la TPSF na majibu ya Profesa Muhongo
Siku ya Agosti 28, 2013 Tanzania Private Sector
Foundation (TPSF) ilifanya kikao chake cha Bodi na baadaye kufanya mkutano na
waandishi wa habari. Mambo mengi yalizungumzwa katika kikao hicho ikiwa ni
pamoja na uwezeshaji wa Watanzania (Economic Empowerment).
Kuhusu uwezeshaji Watanzania, mambo muhimu matatu
yalijadiliwa na kutolewa mapendekezo. Mambo hayo ni 1) Manunuzi ya Umma (Public
Procurement); 2) Ardhi na uvuvi; na 3) suala la gesi asilia.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari, mimi nikiwa
Mwenyekiti wa TPSF, niliwasilisha maoni ya TPSF kuhusiana na Manunuzi ya Umma,
wakati Makamu Mwenyekiti wangu, Salum Shamte, aliwasilisha maoni yetu kuhusiana
na sekta ya ardhi na uvuvi na mwishoni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey
Simbeye, aliwasilisha maoni TPSF kuhusiana na gesi asilia.
Katika maoni yake TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji
wa Watanzania katika uchumi wa gesi na kushauri kusitishwa ugawaji wa vitalu
vya gesi hadi hapo sera ya gesi itakapokua tayari. Mwisho Bwana Simbeye alisema
kwamba TPSF itaomba kukutana na Profesa Muhongo kuwasilisha mawazo na
mapendekezo ya taasisi hiyo.
Siku chache baada ya TPSF kutoa maoni yake mambo
mawili yalitokea. Kwanza Profesa Muhongo alijibu kupitia vyombo vya habari
kwamba mpango wa kugawa vitalu vya gesi na kuingia mikataba utaendelea.
Profesa Muhongo pia alisema wazi kwamba hana mpango
wa kukutana TPSF, kwani kufanya hivyo ni kupoteza muda.
Matokeo yake Profesa Muhongo hajajibu hoja
kuhusiana na barua aliyoandikiwa na TPSF. Binafsi nilishitushwa na msimamo wa
Profesa Muhongo kwani Serikali ya awamu ya nne imepiga hatua kubwa katika kudhihirisha
kuwa ni “serikali sikivu”.
Ingemgharimu nini Profesa Muhongo kukaa na
kutusikiliza? Hakuna ambacho angepoteza zaidi ya dakika chache za muda wake.
Jambo la pili ambalo lilitokea ni mimi binafsi
kushambuliwa kana kwamba maoni yaliyotolewa kuhusiana na gesi ni maoni yangu
binafsi na si ya TPSF.
Mifano ya mashambulizi dhidi yangu ni kama
nilivyoonyesha hapo juu katika email na ujumbe mfupi wa simu (SMS).
Msimamo wa Profesa Muhongo katika gesi ni upi?
Msimamo wa Profesa Muhongo mara baada ya kuteuliwa
kuwa Waziri wa Nishati na Madini ulikuwa ni kutaka kupitishwa kwanza kwa sera
ya gesi asilia kabla ya kuendelea na ugawaji wa vitalu vya gesi.
Septemba 2012, Profesa Muhongo alisema;
“Some of the agreements are really shoddy and
they need to be revoked” and “I can’t
tolerate agreements which are not in the country’s interests but they benefit
a few individuals”.
|
Tafsiri yake ni:
|
“Baadhi ya mikataba ni ya ovyo, na inahitaji kuvunjwa” na “Sitovumilia
mikataba ambayo haina maslahi kwa nchi na inawanufaisha wachache”.
|
Baada ya hapo, Profesa Muhongo aliamrisha Bodi mpya
ya TPDC kusitisha ugawaji wa vitalu vya gesi ambao ulipangwa kufanyika mwezi
Septemba 2012 na kupitia upya mikataba yote.
Profesa Muhongo alinukuliwa
akisema:
|
‘Earlier this month, the state-run Tanzania Petroleum Development
Corporation (TPDC) delayed a licensing round for nine deep-sea oil and gas
blocks previously set for this month until a parliamentary vote on a new gas
policy in October. "Right now as a country, we are in the gas boom and
we don't have gas policy in place.”
|
|
|
[…]
|
|
|
Recent gas strikes off east Africa's seaboard have led to
predictions the region could become the third largest exporter of natural gas
on the planet.
|
|
|
"Our country is reviewing its policy. Is that something
new?" he said. "We want both the companies that are investing in
the country and Tanzanians to benefit from the oil and gas projects."
|
|
|
[…]
|
|
|
"This is completely new business to us. We are learning,"
Muhongo said.’
|
|
Tafsiri yake ni:
|
|
|
|
‘Mwanzoni wa mwezi huu TPDC ilihairisha mchakato wa ugawaji wa vitalu
tisa vya gesi asilia vilivyoko baharini hadi hapo Bunge litakapopitisha sera
mpya ya gesi iliyowasilishwa bungeni mwezi Oktoba;
"Kwa sasa kama Taifa, tuko katika mazonge ya gesi na hatuna sera
ya gesi.
"Nchi yetu inaandaa sera (ya gesi). Hicho ni kitu
kipya?..."
"Tunataka kampuni zote, kampuni zinazowekeza nchini mwetu na
Watanzania tunufaike na miradi ya gesi na mafuta."
"Hii ni biashara mpya kabisa kwetu. Tunajifunza."
|
|
Zoezi wa la kugawa vitalu vya gesi asilia
lilisitishwa lakini hadi sasa matokeo ya kupitia upya mikataba hayajatolewa
hadharani.
Miezi michache baadaye, Februari 26, 2013, Profesa
Muhongo alisisitiza msimamo wake wa kutaka Tanzania kuwa na sera ya gesi kabla
ya kugawa vitalu zaidi. Aliyasema hayo alipokua akihutubia mkutano uliofanyika
Chatham House, mjini London. Mkutano huo uliopewa jina “Tanzania: An Emerging
Energy Producer”.
Ulikuwa na madhumuni ya:
|
“Tanzania is drawing growing attention as a pivotal country in East
Africa for oil and natural gas exploration, having led the region in terms of
new discoveries of natural gas in 2012. With known gas reserves of
approximately 7.5 billion cubic feet, the potential to transform Tanzania's
international standing and domestic electricity production is considerable.
However, recent protests against the construction of a pipeline to Dar es
Salaam highlight the challenges that Tanzania faces in ensuring that the
benefits of its natural resources are widely felt.
|
Tafsiri yake ni:
|
“Tanzania inaonyesha kuja juu katika Afrika Mashariki kwa uvumbuzi wa
mafuta na gesi asilia baada ya kuongoza kwa uvumbuzi wa gesi asilia mwaka
2012. Ikiwa na wastani wa futi za ujazo bilioni 7.5, ni dhahiri itasaidia
Tanzania kupaa katika anga za Kimataifa na kusaidia uzalishaji wa umeme kwa
matumizi ya ndani. Hata hivyo, vurugu za hivi karibuni kupinga ujenzi wa
bomba la gesi kwenda Dar es Salaam inaashiria changamoto mpya ambazo Tanzania
sasa inakabiliana nazo kuhakikisha kwamba manufaa ya gesi asilia yanawafikia watu
wengi zaidi wa chini.”
|
Alichowasilisha Profesa Muhongo katika mkutano huo
kwa ufupi kinapatikana katika tovuti hii;
Kama inavyonekana kwenye kiambatanisho, moja ya
nyaraka aliyowasilisha Profesa Muhongo inaonyesha kwamba mchakato wa kuanza
ugawaji wa vitalu ungeanza baada ya kupitishwa kwa sera ya gesi.
Hadi sasa hatuna sera ya gesi asilia. Lakini jambo la kushangaza, Profesa Muhongo
amebadilika na anataka vitalu vigawiwe kabla ya kuwapo kwa sera gesi.
Sababu za kubadilika kwa Profesa Muhongo hazina
mashiko
Profesa Muhongo amenukuliwa na gazeti la Daily News
la Agosti 31, 2013 akieleza sababu zake za kutaka vitalu vigawanywe kabla ya
kupitishwa kwa sera ya gesi.
Sababu kuu alizozisema ni tatu; (1) Ushindani wa
soko na majirani zetu akitolea mfano wa Msumbiji (2) Sheria ya mwaka 1960
iliyoanzisha TPDC na Sheria ya Petroli ya mwaka 1980 kwamba zinatosha kusimamia
ugawaji wa vitalu akimaanisha sera na sheria mpya zitafuata baada ya ugawaji wa
vitalu; na (3) Watanzania hawana uwezo wa kuwekeza katika sekta hii akimaanisha
waachiwe wageni peke yao.
Maelezo kwamba tunashindana na Msumbiji haya
halalishi ugawaji vitalu kabla ya sera. Utafiti wa gesi asilia ni jambo
linachokua muda mrefu, ndio maana TPDC wanaingia kwenye mikataba ya muda mrefu
(isiyozidi miaka 11 kwenye utafiti na miaka 25 kwenye uchimbaji).
Kwa hiyo
kusubiri miezi michache ili Bunge letu liidhinishe sera, haiwezi kuathiri
ushindani wa kibiashara. Hata nchi Msumbiji anayoizungumzia hivi sasa inapitia
upya mpango wake wa uwekezaji katika gesi asilia na kuingiza sera na sheria
mpya zitakazo simamia rasilimali hiyo.
Katika mahojiano yaliofanyika na jarida
la Africa Report mwezi Julai mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati wa Msumbiji,
Mh. Abdul Razak Noormahomed, alisema madhumuni ya mabadiliko hayo ni kuwapa
kipaumbele wananchi wa Msumbiji.
Mahojiano haya yanapatikana katika anuani ifuatayo:
Kama nilivyoeleza hapo juu, mara baada ya Profesa
Muhongo kuingia wizarani alisema kinaga ubaga kwamba sheria iliyopo haikidhi
mahitaji ya sekta ya gesi asilia ndiyo maana akasimamisha ugawaji wa vitalu vya
gesi na kuamrisha mikataba ipitiwe upya na sera ipatikane. Leo tunashuhudia
Profesa Muhongo akila matapishi yake na kusema kwamba sheria zile zile
alizoziponda sasa zinafaa.
Kauli ya Profesa Muhongo kwamba wafanyabiashara wa
Tanzania wanaweza tu kushiriki biashara ya juisi na soda na hawana uwezo wa
kushiriki katika biashara ya gesi yao ni dharau.
Kigezo gani Profesa Muhongo anatumia kutoa kauli ya
jumla yenye kutawaliwa na hisia? Amefanya utafiti gani kupima uwezo wa kifedha
wa wafanyabiashara wa kitanzania? Kwa taarifa yake, wapo wafanyabiashara wengi
ambao wanaweza kupata fedha kwa ajili ya kuchimba visima vya gesi.
Ni dhahiri kwamba Profesa Muhongo anathamini tu
kampuni za kigeni, anasahau kwamba kuna mifano ya kuwapo kampuni za kigeni
ambazo zimekua zikifanya udalali hapa nchini kwa miaka mingi kwenye rasilimali
za nchi yetu ikiwa ni pamoja na madini na gesi.
Uzalendo wangu:
Ningependa kupuuza tuhuma kwamba mimi si mzalendo
Wantanzania wanafahamu ukweli. Vile vile ningependa kupuuza tuhuma kwamba mimi
ni mbinafsi na sipendi maendeleo ya Watanzania wenzangu kwa hili pia Watanzania
wanafahamu ukweli
Kuhusu Kilimanjaro Hoteli na mgogoro na Yussuf
Manji n.k, mtizamo wako unategemea wewe upo katika kundi lipi kati ya kundi
safi la waadilifu au kundi chafu la wala rushwa. Watanzania wanafahamu msimamo
wangu kwenye hili.
Mimi sipingi kuwepo kwa wawekezaje wageni katika
sekta ya gesi lakini kuna mambo mawili napigania. Kwanza Watanzania wanufaike
na rasilimali yao ya gesi na pili iwepo sera ya gesi inayotoa kipaumbele kwa
Watanzania
Mimi napenda maendeleo ya nchi yangu; kwa hiyo hata
siku moja siwezi kupinga uwekezaji ama ubia na wawekezaji. Ninachosimamia ni
manufaa kwa nchi yangu.
Tuhuma kwamba nafanya kampeni dhidi ya wizara
Tuhuma kwamba nimeandaa kongamano kwa ajili ya
vijana wa Chadema si za kweli. Huu ni uzushi usio na kichwa wala miguu. Vile
vile madai kwamba naitumia vibaya vyombo vya habari vya IPP Media si ya kweli
hata kidogo ikizingatiwa kwamba hata mahojiano ya Profesa Muhongo kwa simu
akiwa Austria, yalirushwa na kituo cha redio cha Radio Stereo kinachomilikiwa
na kampuni yangu ya ITV-Independent Television Limited.
Hitimisho
Julai mwaka huu, Rais wa Marekani Barack Obama,
alihitimisha ziara yake ya Kiserikali nchini Tanzania, kwa kusema;
|
“Ultimately the goal here is for Africa to build Africa for Africans.”
|
|
|
Akimaanisha kwamba, Hatimaye Lengo ni Africa kujenga Africa kwaajili
ya Waafrica
|
|
Profesa Muhongo asipingane na ushauri huu mzuri.
Nimalizie kwa kuwahakikishia Watanzania kwamba
mashambulizi binafsi dhidi yangu yenye nia mbaya ya kunishushia heshima
hayatakaa yafanikiwe.
Wenu,
Dk. Reginald A. Mengi
No comments:
Post a Comment