*************************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea
na kampeni yake ya kusaidia elimu hapa nchini kupitia mpango wake ujulikanao kama shule yetu.
Msaada huo umetolewa katika shule ya sekondari
ya Kasoma ilipo Majita wilayani Musoma mkoani Mara ambapo Airtel imetoa msaada
wa vitabu vya masomo ya sayansi.
Afisa masoko wa Airtel kanda ya Ziwa Bw. Ally
Mashauri amesema, msaada huo unakuja ikiwa ni kuitikia wito wa serikali wa
kusaidia katika masomo ya sayansi nchini.
Afisa Masoko airtel kanda ya ziwa Ally Mashauri
alisema “ Airtel inatambua kuwepo kwa uhaba wa vitabu na vifaa vya
kufundishia katika shule zetu na katika kutatua changamoto hizo tunaongeza
nguvu na kushirikiana na Serikali chini ya wizara ya elimu kuweza kuinua
sekta ya elimu.
Nae Joseph Mushi ni Meneja wa Airtel mkoani mara
anaelezea umuhimu wa msaada huo huku makamu mkuu wa shule ya kasoma Mtaki Bita
akishukuru kwa msaada huo.
“huu ni msaana sana katika kuoneza hari ya
waalimu kufundisha masomo ya mchepuo wa sayansi na pia wanafunzi mkoa huu wa
Mara kupenda kusomea sayansi kwa kuwa nyenzo za kusomea zimepatikana” alieleza Joseph
Mushi meneja airtel Mara
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa shule kasoma
sekondari Mtaki Bita alisema Ninawashukuru sana Airtel kwa uchangia elimu katika mkoa wetu, lakini bado
ninawapa taarifa Airtel na wadau wengine wote kuwa
bado shule yetu inachangamoto nyingi sana ambazo
bado zinahitaji msaada wa wadau wa elimu ili tuijenge Tanzania yetu”
Msaada uliotolewa unahusisha masomo ya kemia,
fizikia, baiolojia na hisabati. Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa
ikitoa misaada mbalimbali ikiwemo ukarabati wa shule, sare za shule, kompyuta
pamoja na kuunganisha baadhi ya shule kwenye mtandao wa internet wa Airtel wa 3.75G
ili kurahisisha wanafunzi kujisomea kupitia mtandao.
No comments:
Post a Comment