Wakati shinikizo la Dunia sasa limeelekea kumaliza tatizo la
ukwepaji kodi na Utoroshaji wa fedha kutoka nchi za Kiafrika, serikali ya Tanzania
inavuta miguu.
Moja ya njia ya Serikali za nchi maskini kupata taarifa za makampuni makubwa ya
kimataifa(MNCs) yanayokwepa kodi ni mfumo wa kupashana taarifa (automatic
exchange of tax information) .
Kufutia shinikizo la nchi mbalimbali, hivi sasa nchi zinazoitwa "secrecy
jurisdictions" (tax havens) Zimeanza kuweka sahihi makubaliano ya kutoa
taarifa. Tanzania
mpaka sasa haijaweka sahihi na serikali haijatoa taarifa yeyote kwa Umma.
Tanzania inapoteza jumla ya dola za kimarekani kati ya milioni 500 na bilioni
1.25 kwa mwaka kutokana na Makampuni makubwa ya kimataifa kukwepa kodi. Hii ni
sawa na kusema Tanzania inapoteza dola takribani milioni mbili kila siku kwa
uporaji huu.
Naitaka serikali kutoa taarifa kwa nini haichuki hatua kuzuia mwanya huu wa
mapato ya Umma. Serikali ichukue hatua mara moja kuhakikisha Tanzania inaingia
makubaliano ya kupashana taarifa za kikodi. Huu sio wakati wa kuvuta miguu
katika suala nyeti la umma. Badala ya kukimbilia kutoza kodi wanyonge,
tuhakikishe makampuni makubwa yanayonyonya rasilimali zetu yanalipa kodi
inayotakiwa.
Waziri Kivuli wa Fedha
24 Oktoba, 2013
No comments:
Post a Comment