Tangazo

May 21, 2012

Tanzania yataka Mfumo wenye kunufaisha Wananchi wa kawaida katika matumizi ya Sekta ya Misitu kupambana na mabadiliko ya Tabianchi

Afisa Misitu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Theodore Silinge (kulia) na Afisa Habari wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Evelyn Mkokoi  wakifuatilia majadiliano ya mjadala wa mabadiliko ya Tabianchi katika kundi la nchi za Afrika kwenye mkutano wa mabadiliko ya Tabia nchi unaoendelea mjini Bonn Ujerumani.
******************************
Na Evelyn Mkokoi, Afisa Habari - OMR
Bonn Ujerumani
Tanzania imetoa na kusisitiza msimamo wake kuhusu haja ya kuanzishwa kwa mfumo bora na wazi kwa ajili ya kugharamia, kufuatilia, kuhakiki na kutoa taarifa kuhusu matumizi ya sekta misitu ili kupunguza uharibifu wa misitu na kuchochea maendeleo kwa wananchi na nchi zinazoendelea.

Msimamo huo umetolewa  leo katika mkutanao wa majadiliano ya mabadiliko ya tabianchi unaendelea hapa Bonn, Germany na Afisa Mazingira ktoka ofisi ya makamu wa Rais Bw. Freddy manyika.

Bw. Manyika ameeleza kuwa jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuandaa makubaliano kuhusu  mfumo wa kugharamia, kufuatilia na kuhakiki na kufuatilia shughuli za kupunguza uharibifu wa misitu na kudhibiti uzalishaji wa gesi joto katika sekta ya misitu kulingana na makubaliano ya Cancun na Durban kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Katika msimamo wake, Tanzania imeisitiza kuwa uanzishwaji wa mfumo huo lazima uzingatie hali halisi na utegemezi wa maisha ya wananchi maskini kwenye sekta ya misitu katika nchi zinazoendelea pamoja na vichocheo vya vyanzo vya uharibifu wa misitu katika nchi hizi.

Aidha Bw. Manyika ameainisha kuwa, Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 80% ya wananchi  wa kawaida Tanzania wanategemea rasilimali ya misitu kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku, hususan kwa ajili ya kujipatia  mahitaji ya nishati ya kupikia,kilimo na usalama wa chakula, ufugaji na fursa mbalimbali za kiuchumi zenye lengo ya kujiongezea kipato na kupunguza umasikini.

“ Zaidi ya 90% ya nishati ya kupikia Tanzania inategemea sekta ya misitu, hivyo ni muhimu mfumo utakaoanzishwa uwe unalenga kusaidia kutatua matatizo hayo kwa kusaidia kuwepo kwa nishati mbadala kwa ajili ya kupikia, kuboresha kilimo ili kuwepo na usalama wa chakula, kujenga na kuimarisha uwezo wa taasisi zinazosimamia sekta ya misitu, kusaidia itakayotumika katika ufuatiliaji wa misitu unapatikanaji wa tecknolojia kwa bei nafuu lisisitiza.’’

Akizungumzia Tanzania kwa niaba ya nchi zinazoendelea kuhusu wakati wa kujadili masuala yanayohusu jinsi ya kutumia sekta ya misitu kukabiliana na mbadailiko ya tabianchi, hususan kwa kupunguza uharibifu wa misitu na kupunguza uzalishaji wa gesijoto katika sekta ya misitu, Bw. Manyika ameeleza kuwa, kuwa pesa za kugharamia utekelezaji wa shughuli hizo hazina budi kutolewa na nchi zilizoendelea kulingana na makubaliano ya mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa makubaliano ya Durban ambayo yametoa fursa kuwa upatikana wa fedha za kugharamia shughuli hizo zinaweza kugharamia shughuli hizo zinatoka kwa sekta za umma na makampuni binafsi, ni wazi kuwa sekta binafsi imejikita zaidi katika kutafuta faida na hivyo ni vigumu kutoa kipaumbele na fedha kwa masuala ambayo hayatoa faida ya moja kwa moja kwa makampuni hayo.

Akitolea Mfano, uboresha miundombinu ya ufuatiliaji, kujenga uwezo wa watumishi katika sekta husika, kuboresha maisha ya mwananchi kwa kuondoa umasikini,  alisema ni vyema uanzishwa mfuko maalumu kwa ajili ya shughuli hizo na kiwango kikubwa cha fedha zitakazotolewa zilenge katika kuboresha maisha na kumnufaisha mwananchi wa kawaida ambaye ndiye huhangaika kila siku kupata riziki yake na kulazimika kuharibu mazingira na maliasili anayoitegemea sana kama misitu.

Aliongeza kuwa,  Jumuiya ya kimataifa ni lazima itambue tatizo la umasikini linalozikabili nchi na wananchi katika nchi maskin, na hivyo kusaidia juhudi za serikali katika kutatua matatizo hayo kwa lengo kuwaleta maendeleo endelevu.

“Mfumo wa kutoa fedha, ufuatiliaji, uhakiki na utoaji taarifa ni lazima ulenge kunufaisha wananchi na nchi zenye misitu badala ya kunufaisha wajanja wachache na makampuni binafsi katika nchi zilizoendelea ambayo mengi  yanajipanga  kutumia fursa hiyo kujinufaisha na kuwanyonya wananchi katika nchi zinazoendelea huku yakiwalaghai kuuza ardhi na misitu yao kwa  bei ya chini na kuwacha hawana ardhi na hivyo kuendelea kuwa maskini zaidi alisisitiza.”

 Pia msisitizo umetolewa kuwa mfumo utakaoanzishwa lazima ufuatilie na kuhakiki pia mwenendo wa utoaji fedha hizo kwa mujibu wa mkataba, makubaliano ya Bali, Cancun pamoja Durban ambayo yanazitaka nchi zilizoendelea kutoa fedha kwa ajili ya kusaidia shughuli za kukabiliana na mbadiliko ya tabianchi kwa nchi zinazoendelea, hususan zenye uchumi mdogo na maskini. Mbali na kuungwa mkono na nchi maskini, msimamo wa Tanzania  pia unaungwa mkono na nchi za Afrika zinazoshiriki katika mkutano huu. 

Mkutano huu wa Mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea Mjini Bonn ni maandalizi ya mkutano mkubwa unaotarajia kufanyika mwezi wa Desemba mjini Doha.

No comments: