Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi |
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza Rais Mstaafu wa
Shirikisho la Mpira nchini (TFF) Leodger Tenga kwa uongozi wa kutilia mfano
uliowezesha kuleta mapinduzi makubwa ya mifumo ya soka nchini.
Aidha CCM inamtumia salam za pongezi za dhati Rais Mpya
wa TFF, Jamal Malinzi, na Uongozi wake wote mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) uliopatikana katika uchaguzi uliofanyika juzi, Oktoba 27, 2013 jijini Dar
es Salaam.
Chama Cha Mapinduzi, kinaimani kubwa na Malinzi wa wenzake katika kuendeleza jitihada zilizoanzishwa na uongozi uliomaliza muda wake sanjari na kuibua mbinu mpya zitakazoboresha na kuleta mapinduzi makubwa ya soka nchini.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye
anawaasa“Tunauomba uongozi mpya kujiepusha na jitihada za kujiendeleza binafsi
na badala yake uwekeze katika soka na kuepusha migogoro isiyo na tija katika
mchezo huo ambao kwa sasa ndio unaopendwa na Watanzania wengi”
“Daima imani huzaa imani, hivyo imani ya CCM kwako na kwa viongozi wenzako mliochaguliwa pamoja izae imani ya utumishi uliotukuka" Ndugu Nape amehitimisha.
“Daima imani huzaa imani, hivyo imani ya CCM kwako na kwa viongozi wenzako mliochaguliwa pamoja izae imani ya utumishi uliotukuka" Ndugu Nape amehitimisha.
Chama Cha Mapinduzi kinatambua kuwa migogoro imekuwa kwa
sehemu kubwa chanzo cha kukwamisha sana maendeleo ya soka hapa nchini na hivyo
kuwanyima Watanzania raha ambayo huitarajia kutoka kwenye mchezo huo na hasa
pale timu zao zinapopata ushindi.
Imetolewa na:-
Kitengo
cha Mawasiliano na Umma
Chama
Cha Mapinduzi
Ofisi
Ndogo ya Makao Makuu
Dar es
Salaam
No comments:
Post a Comment