Tangazo

October 3, 2013

DECI NYINGINE YAZUKA DAR, WENGI WATAPELIWA FEDHA ZAO


Ndugu wanahabari,

Ninaona ninawajibika kuwataarifu kuhusu kuwepo kwa vijana wa Kitanzania ambao wamejiingiza katika mtandao wa kitapeli ambapo wamekuwa wanatangaza kuwa wanatoa mikopo kupitia Kampuni wanayoiita SOCIAL CREDIT COMPANY.

Ili kufanikisha mipango yao wana-hack kurasa za facebook za watu mbalimbali ambao ni maarufu na zile zenye traffic kubwa. Wakifanikiwa wanamwondoa mwenye akaunti kwa kufuta USER NAME na PASSWORD yake na kuimiliki hiyo page. Kinachofuatia hapo ni kuanza kuposti taarifa za ushawishi kwa kutumia jina lako kuwa wewe mwenye akaunti unaijua hiyo kampuni hivyo unawatoa hofu jamaa zako.

Kuna jamaa zangu ambao facebook page yao ilikuwa hacked na kwa sababu kidogo niko kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano nikaanza kuwafuatilia hawa jamaa na kuwataka wenye page watumie neutralizing strategy kwa kuwatumia watu waliokuwa wanaingia mara kwa mara kwenye hiyo page kutuma taarifa za kuitahadharisha jamii juu ya utapeli huu. Ingawa bado wanaishiilia hiyo page lakini zile posti waliziondoa.

Tatizo hili pia liliwapata Airtel kama wiki moja iliyopita, hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa kupitia kiupindi chao cha Power Breafast.

HATUA ZAIDI TULIZOCHUKUA :

Ukisoma kiambatanishi, matapeli hawa wanadai kuwa wana ofisi Mnazi Mmoja na wametoa namba zao za simu na email address. Hivyo vyote ni vya uongo. Aidha, cha kushangaza wamefanikiwa kuandikisha namba za simu za mikononi za mtu wanayemwita Mhasibu wao anajulikana kama MR. ANTHONY SHILLIYE LUCAS. Huyu ameandikisha namba ya MPESA 0756 310 988 kwa jina la ANTHONY SHILLIYE na TIGOPESA  0714 254 735 kwa jina la ANTHONY LUCAS.

Tumetoa taarifa TIGO na VODACOM huku tukiamini kabisa kuwa tutapata ushirikiano wa kumjua mtu anayetumiwa fedha lakini ushirikiano umekuwa mdogo. Pia tumewataarifu TCRA ambao wameahidi kufuatilia kwa sababu huu ni WIZI wa MTANDAO. Hata hivyo mahali pa kuanzia ilikuwa ni kwenye hizi namba za simu kwavile tunaamini usajili wa hizo namba una viambatanisho. Pia kupata taaarifa za wale wote ambao wamekuwa wanawasiliana na hizi namba.

Website yao (http://www.socialcompany.wapka.mobi/index.html) haina kitu zaidi ya hilo tangazo lililoko kwenye attachment ya email hii.

Watanzania wengi waliokumbana na tangazo hilo wamekuwa wanahangaika kutaka kujua ukweli wa Kampuni hii ambayo inadai kufahamika na taasisi nyingi muhimu nchini lakini hakuna. Bado watu wanaibiwa na hili linathibitishwa na post zilizo kwenye hii page ambayo wameifungua wakijifanya ni Wema Sepetu : https://www.facebook.com/wema.sepetu.946?fref=ts.

Kama haitoshi pia wamefungua akaunti ya AirTel Tanzania (https://www.facebook.com/pages/Airtel-Tanzania/438820529559726) ambayo sio akaunti sahihi ya Kampuni ya Simu. Hapo tumekuta post ambayo ipo katika Kiambatanisho kwenye email hii. Utaona Post ati kutoka AirTel wakimtaka Mteja ajaze Fomu.

Tukizingatia umuhimu wa vyombo vya habari katika mustakabhali wa nchi, ninaamini hii habari mnaweza kuitumia kutafuta ukweli wa nini hizi Kampuni za Simu zinajua kuhusu hili? Kwanini hazijoitokezi hadharani kueleza wanachokijua baada ya kupata malalamiko mengi?

Aidha, kwavile huyu mtu anachukua fedha kwa maajenti wa MPESA, TIGOPESA na AirTel Money ina maana hawawezi kusaidia kujua sehemu anayochukulia fedha? Je, kwa kutumia GPS hawawezi kujua huyu jamaa simu zake zinapatikana maeneo gani? Anawasiliana na watu gani? Pia ni IP Address gani anayoitumia kutuma hizo message zake? TCRA ni lazima walijue hili kwani liko katika eneo lao.

Asanteni na samahani kwa kuwachukulia muda wenu mrefu. Ninatumaini mtalipa uzito hili suala ili wananchi wasiendelee kuibiwa na wajanja wachache.

No comments: