Mke wa Marehemu, Maria Kombe (katikati) pamoja na watoto wake wakifuatilia ibada ya Maziko ya Mume wake, aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. |
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama (katikati), Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz (kulia) na Kaimu kamanda wapolisi mkoani Kilimanjaro, Moita Koka, wakitoa heshima za mwisho katika Jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. |
Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, ukiondolewa kanisani katika kanisa la KKKT, usharika wa Msae kuelekea Nyumbani kwake kwa ajili ya zoezi ya Maziko yaliyofanyika Jana, kijijini Msae, kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoani Kilimanjaro. |
Askofu Mkuu wa KKKT kanda ya Kaskazini, Dkt. Martin Shao, akiweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. |
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, akiweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. |
Kamanda wa Polisi kilimanjaro, Robert Boaz na Kamanda wa Polisi Arusha, Liberatus Sabas (mwenye suti) wakiweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. |
Mke wa Marehemu, Maria Kombe, akiweka Ua katika Kaburi la Marehemu mume wake, aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. |
Wanafamilia wakiweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. |
Watoto wa Marehemu Kombe, wakiongozwa na Kaka yao, Dustan Kombe kuweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. |
Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Aisha Nyerere, akiweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. |
Vijana wa Jeshi la Polisi, wakitoa Heshima za mwisho katika
kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, kwa Mujibu waTaratibu
zaKijeshi. Kombe alizikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro. picha zote na Taifa Letu.com blog Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, amewaongoza Maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya Aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna mstaafu, James Kombe (63), aliyefariki dunia October 21 mwaka huu katika Hospitali ya Ocean Road, jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kombe aliyeitumikia Jeshi la Polisi kwa muda wa miaka 24, katika nyadhifa mbalimbali, alizikwa jana saa 9:40, alasiri, Nyumbani kwake katika kijiji cha Msae, kata ya Mwika, Jimbo la Vunjo, wilaya ya Moshi vijijini, mkoani Kilimanjaro baada ya ibada ya maziko iliyofanyika katika Usharika wa Msae-Lyakrima na kuongozwa na Askofu Mkuu wa KKKT, dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Martin F. Shao. Akitoa Salamu za Rambirambi, Gama alisema serikali imeguswa na msiba huo huku akimuelezea Marehemu Kombe kama mtu muadilifu, mwaminifu na mtu asiyekuwa, asiyekuwa na ubinafsi na mzalendo aliyeitumikia Taifa lake kwa nguvu zake zote hadi dakika za mwisho za uhai wake. “Ni kweli mazingira yetu kikazi yanatofautiana, lakini ni wazi kuwa kuna mengi ya kujifunza na kujivunia kutoka kwa Kamishna Kombe enzi za uhai wake, Marehemu ameacha historia iliyotukuka nyuma yake, alikuwa ni mtu mwadilifu sana, mwaminifu, mzalendo na mchapa kazi aliyejitoleakulitumikia Jeshi la Polisi na Taifa kwa ujumla,” alisema Gama. Kuhusu swala la uwajibikaji na utendaji kazi, Gama alisema wananchi wengi kwa sasa wanashindwa kufanya kazi za maendeleo hasa mkoani Kilimanjaro katika maeneo ya Rombo, Marangu na Mwika kutokana na kukithiri kwa vitendo vya Unywaji pombe holela ambapo aliagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia na kudhibiti hali hiyo. Awali akiongoza Ibada ya Maziko, Askofu MKuu wa KKKT, dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Martin Shao, aliwataka waumini wa dini ya Kikristo, wananchi pamoja na watumishi katika Jeshi la Polisi kufanya yale yaliomema ikiwa kweli wanataka kuenziwa kama ilivyo kwa Marehemu Kombe. Dkt. Shao katika ibada hiyo alimuelezea Marehemu Kombe kama mtu anayestahili kuenziwa daima kama anavyoenziwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutoka na utendaji wake kazi uliotukuka, uzalendo na Uadilifu pamoja na uwajibikaji katika kuhakikisha Amani ya Tanzania na usalama wa Wananchi wake. Kabla ya kifo chake, Kamishna Kombe, alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Kansa ambao ulianza kumsumbua Juni mwaka jana na kutibiwakatika Hospitali ya Rufaa KCMC mjini Moshi. James Kombe, aliyezaliwa mwaka 1950, mwika Kilimanjaro ameacha mjane mmoja, Maria Kombe na watoto watano na kwamba alilitumikia Jeshi la polisi kuanzia Machi, mwaka 1970 na kulitumikia mpaka alipostaafu mwaka 2010. Akisoma historia ya Marehemu, Kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani, Joseph Mwakabonga alisema Kamishna Kombe, alijiunga na Mafunzo ya awali machi 23 mwaka 70 na kumaliza Agosti 28 mwaka huo, huko Mopshi baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1969 nchini Uganda. Alisema alipandishwa vyeo kama Mkaguzi wa polisi (1977), Kamishna msaidizi (1995), Mkaguzi wa polisi (1986), mrakibu mwandamizi (1991) na Kamishna Msaidizi wa Polisi (2002) hadi alipostaafu 2010. |
No comments:
Post a Comment