***************
Na Mwandishi wetu
USAJILI kwa watu wanaotaka
kushiriki mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon, zinazotarajiwa
kufanyika Desemba 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam umeanza rasmi.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya mbio hizo, Innocent
Melleck alisema, mara baada ya Dar es Salaam fomu za usajili zinatarajiwa
kutolewa Dodoma kuanzia wiki ijayo.
“Tunapenda kutangaza rasmi
kwamba usajili kwa ajili ya mbio hizo umeanza rasmi katika Mkoa wa Dar es
Salaam, ambapo kuna vituo zaidi ya 13 vilivyofunguliwa katika maeneo
mbalimbali.
“Pia siku ya Jumanne na
Jumatano wiki ijayo fomu hizo zitatolewa rasmi katika Viwanja vya Bunge, Dodoma
ambapo Spika Anne Makinda ndiye anayetarajiwa kuongoza katika kujisajili.
“Kingine mtu anayetaka
kushiriki anaweza pia kujisali kwa njia ya mtandao wa internet na tunafanya
utaratibu maalumu wa kuhakikisha pia yoyote anayetaka anaweza kujisaili kwa
njia ya simu, “ alisema.
Melleck alisema, katika
usajili huo, fomu zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000
yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh
6,000.
“Pia tunapenda kuchukua fursa
hii kuziomba kampuni au taasisi mbalimbali zinazotaka kudhamini mbio hizo
zijitokeze na kufanya hivyo, kwani nafasi bado ipo na tukumbuke bila amani
hakuna chochote kinachoweza kuendelea, hivyo hata wao pia wanatakiwa kuipigania
amani kwa nguvu zote.”
Mbio hizo zinatarajiwa
kushirikisha wanariadha kadhaa maarufu duniani.
No comments:
Post a Comment