Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (katikati), akiwasiliana kwa simu na Rashid Jacob Kagomola mkazi wa Bukoba
mkoani Kagera aliyeibuka mshindi wa pili wa tiketi mbili na safari ya kwenda
kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) nchini
Uingereza kwenye uwanja wa Old Trafford, wakati wa droo ya wiki ya pili ya
‘Mimi Ni Bingwa’ iliyochezeshwajijini Dar jana. Kulia ni Ofisa Huduma Kwa
Wateja Airtel, Pamela Marinyo na Emmanuel Ndaki, Msimamizi Mwandamizi wa Bodi
ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.
#####################
Kagomola
aibuka mshindi wa tiketi ya pili ya Airtel kwenda Old Trafford
KAMPUNI
ya mawasiliano ya Airtel imemtangaza Rashid Kagomola, mkazi wa Bukoba mkoani
Kagera kama mshindi wa tiketi mbili na safari iliyolipiwa ya kwenda kuangalia
moja kwa moja (live) mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza katika uwanja wa Old
Trafford.
Kagomola
alishinda safari hiyo wakati wa droo ya kila wiki ya promosheni ya ‘Mimi Ni
Bingwa’ inayolenga kuwazawadia wateja waaminifu, iliyoingia katika wiki ya
pili. Anakuwa
mshindi wa pili wa tiketi baada ya Dickson Lyatuu kutoka mkoani Arusha, kuibuka
mshindi wa kwanza.
Akitangaza
mshindi wa tiketi hiyo katika wiki ya pili, washindi wawili wa shilingi milioni
5 na washindi wanne wa shilingi milioni moja kila mmoja, Meneja Uhusiano wa
Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema washindi wote wa tiketi watapewa
nafasi ya kuchagua mtu mmoja watakaesafiri nae kwenda Uingereza, kuangalia
mechi ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford.
“Tunafuraha
kutangaza kuwa mshindi wetu wa tiketi ya kweneda Old Trafford wa droo yetu ya
pili ya promosheni ya ‘Mimi Ni Bingwa’ kuwa ni Rashid Jacob Kagomola
atakaeungana na Bw. Dickson Lyatuu aliyeshinda tiketi ya kwanza na wengine 11
watakaojishindia tiketi baadae kwenda kuangalia mechi moja kwa moja (live)
katika uwanja wa Old Trafford katika mwezi huu wa kwanza wa droo yetu.
“Kagomola
alichaguliwa baada ya namba ya mtu wa kwanza kujitokeza, kushindwa kupokea simu
baada ya kumpigia mara tatu. Kwa maana hiyo napenda kumuasa kila aliyejisajili
katika droo hii kujiweka tayari kupokea simu kutoka Airtel kwa sababu anaweza
kuibuka mshindi,” alisema Mmbando.
Aliwataja
Godfrey David Msiu kutoka Arusha na Junior Ashery Pesambili, mkazi wa Arusha
mjini kuwa washindi wa shilingi milioni tano kila mmoja wa wiki hii na wateja
wengine wanne waliojishindia shilingi milioni moja kila mmoja.
Mmbando
alisema kuwa bado zawadi nyingi zaidi kushindaniwa na kuongeza kuwa ili
kushiriki katika promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS)
ukiwa na neon “BINGWA’ kwenda namba 15656.
Alisema
kuwa Airtel pia imeweka vituo maalum kwa ajili ya wapenzi wa Man U kuangalia
mechi za Manchester United bure kupitia luninga kubwa, na kuyataja maeneo hayo
kuwa, Mbeya – Shaba Pub, Mwanza – Shooters Pub, Dodoma – Four Ways, Dar es
Salaam – Rose Garden, Morogoro – Nyumbani Lounge na mkoani Arusha ni Empire Sports
Bar.
Droo
hiyo ilishuhudiwa na wawakilishi kutoka katika Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment