Waziri Mkuu Mizengo Pinda |
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Mtwara
Mradi wa uzalishaji gesi asilia umeonesha kuwa ni kichocheo kikuu na muhimu katika kuleta na kuinua sekta ya viwanda nchini kwa manufaa ya taifa na wananchi wake.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili katika mikoa ya Lindi na Mtwara hivi karibuni alipokuwa akitembelea mikoa hiyo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba la kuisafirisha gesi asilia kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam.
“Ujenzi wa viwanda vya vya saruji vya MEIS kilichopo kijiji cha machole mkoani Lindi na Dangote kilichopo kijiji cha Msijute mkoani Mtwara unaoendelea ni dalili nzuri na njema kwa nchi na maendeleo ya na watu wake” alisema Waziri Mkuu Pinda.
Ujenzi wa viwanda hivi unaoendelea umefikia hatua mbalimbali ni matokeo ya kugunduliwa gesi asilia katika mikoa hiyo ambapo itakuwa ndio chanzo kikuu cha nishati ya umeme katika viwanda hivyo.
Waziri Mkuu Pinda alisema kuwa viwanda hivi vitanufaika na umeme wa kuendeshea uzalishaji wa saruji katika viwanda hivyo ambao chanzo chake kikuu ni gesi inayopatikana katika mikoa hiyo.
Ili kuhakikisha viwanda hivyo vinapata umeme wa uhakika Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alisema kuwa gharama ya kuunganisha umeme kwa wananchi nchini imepungua katika maeneo mbalimbali nchini.
Prof. muhongo alisema kuwa kwa sasa maeneo ya vijiji vyote vya mikoa ya Mtwara na Lindi wamepewa ofa maaluum ya kuunganishiwa umeme kwa gharama ya sh. 99,000/= za kitanzania ofa ambayo itaisha mwezi Juni mwa huu ikilinganishwa na gharama ya mwanzoni ambapo nchi nzima wananchi waishio vjijini bado wanaendelea kuunganishiwa umeme kwa sh. 177,000/=.
Wananchi wa maeneo hayo wamehimizwa kuchangamkia fursa hii iliyotolewa na serikali ili kuboreha maisha yao hasa katika karne hii ya sayansi na teknolojia.
Waziri Pro. Muhongo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi wanaoishi karibu na bomba la kusafirishia gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam wamepunguziwa zaidi gharama ya kuunganisha umeme kwa sh.27, 000/= za kitanzania.
Muhongo amesisitiza kuwa hakuna serilkali yeyote duniani inayotoa huduma ya kuunganishiwa umeme kwa bei ndogo kama hii.
Waziri Muhongo amaeendelea kusema kuwa wananchi waishio mijini nao wamepewa fursa hiyo ya kujihakikishia kuunganishiwa nishati hiyo kwa gharama ya sh. 330,000/= za kitanzania.
Kutokana na uhakika wa nishati hiyo katika viwanda vya saruji vya MEIS na Dangote, wakazi wa maeneo yanayozunguka viwanda hivyo na watanzania kuwa ujumla watanufaika na kujengwa viwanda hivyo ambapo zaidi ya wananchi 70000 wataajiriwa.
Naye Mkurugenzi Mendaji wa Kiwanda cha saruji cha MEIS Merea Barabuu alisema kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kukamilika mwaka huu ifikapo Desemba kwa kuwa vifaa vyote vimekamilika na vipo tayari.
Barabuu alisema kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha takribani tani 500 hadi 700 kwa siku ambapo kwa mwaka ni sawa na tani 200,000 hadi 250,000 ambapo malighafi zote za kuzalisha saruji zinapatikana ndani ya mkoa wa Lindi.
Katika ziara hiyo Waziri Mkuu katika msafara huo aliambatana Mke wake Mama Tunu Pinda,Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) Hawa Ghasia, watumishi wa wizara ya Nishati na Madini, watendaji wa shirika la TPDC, viongozi wa shirika la umeme TANESCO na wabuge wa maeneo ya mikoa hiyo.

No comments:
Post a Comment