Tangazo

February 17, 2014

UNIC YAHAMASISHA VIJANA MKOANI DODOMA KUANZISHA VILABU VYA UMOJA WA MATAIFA MASHULENI

DSC_0029
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama, akibadilishana mawazo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kikuyu Mwl. Zaituni Mkoyi alipotembelea shuleni hapo kwa lengo la kuwahamasisha wanafunzi kuanzisha vilabu vya Umoja wa Mataifa. Katikati ni Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo Bw. Francis Tumaini.
DSC_0032
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama, akisaini kitabu cha wageni cha shule ya Sekondari Kikuyu iliyopo mkoani Dodoma.
DSC_0081
Afisa habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama, akizungumza na vijana wa shule za sekondari Kikuyu iliyopo mkoani Dodoma, kuwaelezea umuhimu wa kujiunga na vilabu vya Umoja wa Mataifa (UN Clubs) vinavyoanzishwa mashuleni kwa lengo la kuwasaidia kujitambua na nafasi yao kama vijana katika kutekeleza agenda mbalimbali za Umoja wa Mataifa.

Bi. Ledama amefafanua kuwa, kuanzisha vilabu hivyo shuleni hapo kutawawezesha kujifunza shughuli za Umoja wa Mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kuisaidia jamii zao kupitia program mbalimbali ikiwemo na masuala ya Kidiplomasia.

Bi. Usia pia amewafafanulia vijana hao kuwa katika klabu hizo wataweza kuwa na mtandao na vijana wengine kitaifa na kimataifa, kupata nafasi ya kufanya kazi za kujitolea.

Pia amewagusia suala la kujiepusha na marafiki wenye tabia mbaya itakayowapelekea kujihusisha na vitendo visivyo vya kimaadili ikiwemo uvutaji bangi na matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo ni moja ya changamoto kubwa inayoikabili Tanzania kwa sasa, aidha amewasaa kutojihusisha na ngono pindi wawapo mashuleni ili kujiepusha na gonjwa hatari la Ukimwi. (Pichani kushoto ni Mwalimu Cecilia Mwolo na Mwalimu Elias Ndangula na Kulia ni Bw. Laurean Kiiza kutoka UNIC Dar es Salaam).
DSC_0059
Mmoja wa wanafunzi shule ya Sekondari Kikuyu akiuliza swali kwa Afisa Habari wa Kitengo cha Habari (UNIC) hayupo pichani.
DSC_0084
Sehemu ya Wanafunzi vidato mbalimbali wa shule ya Sekondari Kikuyu wakimsikiliza Bi. Usia Nkhoma Ledama.
DSC_0043

No comments: