Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa
Christophe Soulet akikata utepe kuzindua duka la Airtel lililopo
mlimani city jijini Dar es Saalam.wakishuhidia,wapili ni Andre Beyers
Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja wa duka Wahida Saleh na
Sunil Colaso Mkurugenzi Mkuu Airtel Tanzania.
XxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxX
Dar es
Salaam
Airtel Tanzania mwishoni mwa wiki hii
imezindua duka la Mlimani City baada ya kulifanyiwa matengenezo na
kulipatia sura ya kisasa zaidi. Uzinduzi huu ni kielelezo cha kampuni hiyo
kutoa huduma bora za simu kwa wateja wake.
Akiongea wakati wa uzinduzi
Christophe Soulet, Afisa Mtendaji Mkuu Africa alisema” Airtel tunaamini katika
kutoa huduma bora za kisasa zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu huku
tukiwapa uzoefu wa pekee katika hudumazetu. Mpango huu wa kuboresha
maduka yetu unafanyika katika masoko yetu yote yaliyoko barani Afrika na Leo
ninayofuraha kuzindua duka hili la kisasa lijulikanalo kama Express shop hapa
nchini Tanzania.
Duka hili la kisasa linathibitisha
dhamira yetu ya kutoa huduma bora Tanzania na Afrika kwa ujumla
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema” duka hilo ni la kwanza kuzinduliwa kwani tunabadilisha maduka yetu yote nchi nzima na kuyafanya yawe na mtazamo mpya na wa kisasa zaidi. Duka hili limetengenezwa na kuhakikisha mteja ataweza kupata huduma kwa haraka , kwa usalama bila usumbufu wowote.
Aliongeza kwa kusema Airtel inapenda kuwahakikishia wateja kupata huduma bora wakati wote na pia kupata simu za aina mbalimbali ambazo zitapatikana katika duka hilo jipya la Mlimani City.
Kwa kupitia mtandao wetu mpana ulionea zaidi tunawahakikishia wateja wetu huduma bora za kisasa, za uhakika jijini Dar es salaam.
Duka la Mlimani City litaendelea kuuza
bidhaa mbalimbali kama vile modem na simu za aina mbalimbali , wateja
watapata huduma ya Airtel money kwa usalama zaidi , kuunganisha na huduma za
simu za malipo ya mwenzi na ya awali , pamoja na huduma za internet na
kuunganishwa na mtandao na kuperuzi kwenye internet , kununua muda wa
maongezi pamoja na huduma nyingine nyingi.
Airtel Tanzania inaendele kuboresha huduma zake kwa wateja ambapo inaendele kuboresha maduka yake nchini nzima kwa mwaka huu wa 2014. Mpango ni kuwafikiwa wateja wengi zaidi na kuboresha huduma zake kupitia maduka yake yote yaliyoko nchi nzima.
No comments:
Post a Comment