Tangazo

July 25, 2014

Rais Kikwete aongoza Watanzania katika Siku ya Mashujaa jijini Dar

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kasimama kikakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka ngao kwenye mnara wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo. Wengine ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Waziri Mkuu Mzengo Pinda leo Julai 25, 2014.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Frederick Sumaye kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo. Wengine toka kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe Mohamed Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar  Mhe omar  Othman makungu leo Julai 25, 2014.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiamkiana na wazee wa Tanzania Legion waliopigana katika vitra kuu ya dunia ya pili waliohudhuria  kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani  ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014. PICHA NA IKULU

No comments: