Tangazo

July 22, 2014

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS KAZI MAALUM PROF. MARK MWANDYOSA AFANYA ZIARA YA KIKAZI MAKAO MAKUU YA TCAA JIJIJI DAR

Kaimu Mkurugenzi Mkuu , Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)  Dk.  james Diu( Kulia ) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya  wakati alipotembelea  makao makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kujionea shughuli zinazofanywa na TCAA.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum , Prof Mark Mwandosya akikabidhiwa  Nyaraka ya Sheria  ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA  na  Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka hiyo  Dk. James Diu , wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya ofisi hiyo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa hapo.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum , Prof Mark Mwandosya, akisisitiza jambo  kuhusiana na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakati alipokutana na Uongozi wa  Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu , Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)  Dk.  James Diu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kiusalama wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),  akifafanua wakati wa ziara ya  Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya  Makao Makuu ya TCAA  jijijni Dar es Salaam.
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  na Mamlaka zingine za Udhibiti Nchini wakati alipotembelea Makao Makuu ya TCAA, Dar es Salaam.
Meneja  Mahusiano wa  Mamlaka ya Udhibiti  Usafiri wa  Nchi Kavu  na Majini –(SUMATRA),  David Mziray akifafanua jambo wakati wa ziara ya Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya  TCAA makao makuu.

No comments: