Mkuu wa wilaya ya Uvinza Khadija Nyembo (katikati), kabla ya kuzungumza na wananchi wakati wa uzinduzi huo. |
Kikundi cha Ngoma za
Utamaduni kikiburudisha wananchi wakati wa hafla ya uzinduzi wa mnara wa Airtel katika Kijiji cha
Sigunga wilaya ya Uvinza mkoani
Kigoma mwishoni mwa wiki.
XXXXXXXXXXXXXXXXX
· Yazindua mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Sigunga mkoani
Kigoma, wanakijiji Kunufaidika na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi toka
Airtel
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua rasmi
huduma za mawasiliano katika kijiji cha Sigunga wilaya ya Uvinza mkoani
Kigoma
Uzinduzi huo unafatia jitihada za kampuni ya Airtel kuendelea
kuboresha mawasiliano ya huduma za simu za mkononi katika maeneo mbalimbali
nchini husasani katika maeneo ya vijijini huku lengo likiwa ni kuzifikia jamii
zinayoishi pembezoni mwa nchi huduma bora ya Airtel Money.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma za mawasiliano
Sigunga, Meneja Mauzo kanda ya Ziwa bwana Raphael Daudi alisema “ Airtel
inatambua adha wanayoipata wakazi wa kijiji cha Sigunga na maeneo ya jirani
katika kupata huduma za mawasiliano kwa muda mrefu sasa, hivyo tumeonelea
ni vyema basi tukachukua hatua ya kuboresha huduma hizi muhimu kwa kuwafikishia
wanakijiji hawa mawasiliano yatakayowawezesha kufanya shughuli zao za
kila siku kwa ufanisi zaidi
Kupitia mnara huu sasa tunaweza kuwaunganisha wanakijiji hawa na
maeneo mengine ya nchi, tutawawezesha kupata masoko ya kuuza biashara zao kwa
urahisi, tumewawezesha kupata huduma za kifedha kupitia huduma yetu ya Airtel
Money ambapo sasa wataweza kupokea na kutuma pesa kwa ndugu jamaa na marafiki
pia kupokea malipo ya biashara zao na kuweza kufanya malipo mbalimbali ya
huduma muhimu wakiwa majumbani mwao. Sambamba na hilo mawasiliano jijini hapa
yamekuwa chachu ya maendeleo na ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa ujumla.
Kwa upande mkuu wa wilaya ya Uvinza Khadija Nyembo alisema”
Tunawashukuru sana Airtel kwakutambua kwa vitendo umuhimu wa mawasiliano kwa
kutufikishia mawasiliano kijijini hapa. Kupitia mawasiliano ya Airtel tumeweza
kuboresha usalama wa raia na mali zao, kuwezesha kufanyika kwa shughuli
za kiuchumi kiufani , wakulima sasa wanauhakika wa kupata masoko na kupata
malipo kwa kupitia simu ya mkonono. sambamba na hilo mawasiliano hayo
yamewezesha huduma muhimu za kijamii kuboreshwa zaidi.
Natoa wito kwa wakazi wa Sigunga Na vijiji vya jirani kutumia
mawasiliano haya katika kukuza uchumi wao na wa jamii kwa ujumla.
Wakiongea kwa wakati tofauti wakazi wa Sigunga wameishukuru Airtel
kwa kuwafikishia mawasiliano hayo nakusema , tumekuwa na adha kubwa ya
huduma za simu kabla ya mawasiliano haya kufikishwa kijijini hapa lakini kwa
sasa kero hiyo imekwisha kabisa hivyo tunaipongeza sana kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel kwa juhudi zao.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Airtel Provides
communication Services to residents of Sigunga, Kigoma
· Launches a communication tower at Sigunga area in Kigoma.
Residents to enjoy ranges of products and services from Airtel
Airtel Tanzania has officilally unveiled
communication services at Sigunga Village in Uvinza district Kigoma today.
The launch is a continuation of Airtel’s efforts
to develop communication services in various areas of the country particularly
rural areas so as to reach societies living on the country’s subdued regions.
“Airtel has identified the hassle caused due to
the lack of communication facilities at Sigunga residents and neighboring areas
for a long time. We have taken the responsibility to facilitate
communication service in order to improve these vital conveniences to the people
of Sigunga village and enable them to engage in their daily activities with
more efficiency”, said Mr. Raphael Daudi, Lake Zone sales manager at the launch
event.
Additionally Daudi said, “Through this
communication tower, we can connect Sigunga residents to the world, enable them
to easily obtain markets for their businesses and give them access to financial
service through Airtel Money service, send and receive money from family and
friends. Moreover, they can make payments for business and household requirements
at their home comfort.”
On her part Uvinza district commissioner Khadija
Nyembo said, “We thank Airtel for providing us with telecommunication services
here in Sigunga. We have witnessed significant improvement in the social
services through Airtel communication services. Now security for residents and
their assets has being improved, economic activities will be performed
effectively, farmers will now be able to market their products, receive
information, sell their products and receive payments through their cellular
phones. . Furthermore these amenities will greatly improve social services.”
“I call upon Sigunga residents and neighboring
villages to use these services for the growth of their economies and the
society as a whole.” Added Nyembo.
Speaking at different periods, Sigunga residents
have thanked Airtel for providing these services, stating that the lack of
communication has been a big nuisance before the introduction of the
facilities, but now such trouble has been ended, and we congratulate Airtel
Telecommunications Company for their efforts.
end
No comments:
Post a Comment