Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na watoto wa
marehemu pamoja na Jaji Mstaafu Mark Bomani alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa
aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu,
Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki katika
Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam Agosti 19, 2014.
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia Salamu za Rambirambi
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, National
Electoral Commission (NEC) kufuatia taarifa
za kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu, Mheshimiwa
Lewis Makame kilichotokea katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es
Salaam tarehe 18 Agosti, 2014.
“Nimepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa
Tanzania na Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) chini ya
Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa, Mheshimiwa Lewis Makame ambaye amelitumikia
Taifa letu katika Utumishi wa Umma kwa uaminifu, uadilifu, bidii na umahiri
mkubwa”,
amesema
kwa masikitiko Rais Kikwete katika Salamu zake.
Katika
utumishi wake, Marehemu Jaji Lewis Makame, enzi za uhai wake, alikuwa Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania kabla ya kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa na baadaye Mwenyekiti
wa NEC ambayo aliiongoza kwa miaka 17 mfululizo hadi alipostaafu mwaka 2011. Uongozi wake ulichangia sana kuimarisha amani,
utulivu, umoja na mshikamano wa kitaifa katika mazingira mapya ya demokrasia ya
vyama vingi vya siasa hapa nchini.
“Ni
kwa kutambua kipaji kikubwa cha uongozi alichokuwa nacho Marehemu Jaji Lewis
Makame, Taifa letu limepoteza mtu muhimu sana kwani hata baada ya kustaafu
kwake alikuwa bado anahitajika sana kutokana na mchango wake wa ushauri katika
mambo mengi yanayohusu maendeleo ya nchi yetu”, amesema
Rais Kikwete na kuongeza,
“Kutokana
na msiba huu mkubwa, nakutumia Salamu za Rambirambi kwa kumpoteza aliyekuwa
Kiongozi Mahiri wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kupitia kwako, naomba Salamu
zangu za Rambirambi na pole nyingi ziifikie Familia ya Marehemu kwa kumpoteza Kiongozi
na Mhimili Madhubuti. Namuomba Mwenyezi
Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu,
Jaji Lewis Makame, Amina”, amesema Rais Kikwete
akiomboleza msiba huu.
Amewahakikishia
Wanafamilia kuwa yuko pamoja nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa, na
anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema awape moyo wa uvumilivu, ujasiri na
subira Wanafamilia wote, ndugu na jamaa wa Marehemu, ili waweze kuhimili
machungu ya kuondokewa na Mpendwa wao kwa kutambua kuwa yote ni Mapenzi yake
Mola.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
19 Agosti,
2014
|
August 20, 2014
RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA JAJI LEWIS MAKAME
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment