Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda
akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua duka jipya la
Airtel liliko mkoani Mtwara mtaa wa maduka mwishoni mwa wiki hii, Airtel
tayari imeshazindua maduka 10 kaika mikoa tofauti tofauti kwa lengo la
kubosresha huduma.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
MTWARA
KATIBU
Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda, ameipongeza kampuni ya simu za
mikononi ya Airtel kwa kuboresha mazingira ya maduka yao kuwa ya kisasa
na kiusalama zaidi kwa watumiaji wa huduma zao mbalimbali hususani ya
Airtel Money.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa duka hilo ambalo liko katika mtaa
wa Maduka Makubwa mjini hapa, Luanda, alisema kuwa kufunguliwa kwa
duka hilo litawahakikishia wateja wao kwa usalama zaidi wanapofanya
miamala ya fedha kupitia counter maalumi zilizowekwa kwa ajili ya
kuhakikisha usalama wa wateja na mali zao kwa ujumla na pia kutaleta
huduma karibu kwa wateja wao kwa wakati muhafaka na .
“Tunaposema
maendeleo ni matokeo lakini vichocheo hivyo vinaletwa na vitu vingi sana
na leo hii tunaona ni namna gani munavyowasaidia wateja wanu…kwa mfano
zamani mtu alikuwa anatoka Mtwara kwenda Kilombero huku amebebelea hela
kwenye mfuko anafika njiani unakuta gari inavamiwa na majambazi na anapolwa
fedha zake zote… lakini sasa hivi mtu anaweza kuwekaa tu kwenye simu
anafika huko ananunua tu mpunga wake na kurudi bila kupata tatizo lolote
sijui wapole mpunga lakini
hii yote inatokana kwa ajili ya mabadiliko makubwa katika mitandao
yetu,” alisema na Luanda na kuongeza:
“Airtel
mko katika ngazi ya juu kuhakikisha kwamba mabadiliko haya yanakuwa
kweli na sisi wateja wenu yatatufanya Tuwaamini sana…mimi ninachoomba
sana muitangaze sana Airtel kwa wananchi ili wajiunge na huduma
yenu na wasipoelewa munawaelimisha ndio biashara na pia mpanue huduma
zenu muende sehemu nyingi za vijijini kwa sababu jinsi mnavyokuwa wengi
wananchi wanapata huduma kwa karibu na kwa haraka zaidi,” alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana
Lyamba, alisema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo kwa mkoani hapa litaendelea
kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Airatel na wanaweza wakazipata
mahari hapo kwa watu wa mikoa ya Lindi na Mtwara.
“Kama
mnavyojua hivi sasa kila siku teknolojia inazidi kupanuka na imekuwa
ikibadilika na la msingi tunawasisitizia wateja wetu kuendelea kutumia
mtandao wetu wa Airtel kwani mpaka sasa tuna mikakati wa kuzindua maduka
yetu zaidi ya kumi na moja kwa ajili ya kuwawezesha wateja wetu kupata
huduma zetu mbalimbali kwa haraka na wakati muhafaka.
No comments:
Post a Comment