Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Marie Stopes Tanzania (MST), Uller Muller (kulia) akikabidhi
kisanduku chenye vifaa vinavyohusika na masuala ya uzazi wa mpango kwa
Balozi mpya wa Marie Stopes ambaye pia ni msanii mkongwe wa muziki wa
kizazi kipya, Judith Wambura 'Lady jaydee' katika hafla ya utiaji sahihi
makubaliano hayo katika ofisi za MST, jijiji Dar es Salaam jana.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam
Lady Jaydee, mwana
muziki mashuhuri wa kizazi kipya nchini Tanzania, aliibua shangwe na chereko
kwenye hospitali ya uzazi Marie Stopes iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.
Uwepo wa Jaydee
ulitokana na kuungana kwa nyota huyu na Marie Stopes kwenye kampeni ya “Chagua
Maisha” ambayo inalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa
mpango katika jamii.
Akiongea na waandishi wa
habari punde baada ya mazungumzo na Mkurugenzi Msimamizi wa MST nchini
Tanzania, Bi Uller Muller, Lady Jaydee aliwaambia waandishi : “Nina furaha
kubwa kuchukuka nafasi hii ya kipekee kama Balozi wa Marie Stopes kwa sababu
wanafanya mengi kuwawezesha wakina mama kusimama na kujitegemea.
Lengo kuu la Kampeni hii
ya Chagua Maisha nikuhakikisha kila Mtanzania ana haki ya kuchagua mfumo wa
uzazi wa mpango ili kulinda afya zao na kutimiza malengo yao ya kimaisha,
hususan mabinti wadogo”.
Akitafakari sababu
zilizompeleka kuungana na kampeni hii, Lady Jaydee alieleza: “siku zote
nilikuwa naamini kuwa wanawake wana uwezo wa kubadilisha Tanzania kimaendeleo.
Hivyo niliumizwa moyo sana nilipoambiwa hivi leo kuwa Wanawake wengi hupoteza
maisha, na wasichana wengi wanalazimishwa kuacha masomo kutoka na ujauzito.
Mimi nimeamua kusaidiana na Marie Stopes kuelimisha jamii nzima wanaweza kubalili
fikra na hatima zao, kwa kutumia uzazi wa mpango”.
Takwimu zinaonyesha
kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kwenye idadi ya vijana, 54%
wakiwa chini ya umri wa miaka 20. Vijana hawa wana uwezo wa kubadili na kukuza
hali ya kiuchumi ya Tanzania ndani ya miaka 10 ijayo iwapo watapata msaada.
Akiwa amesimama Pamoja
na Lady Jaydee, Bi Muller alikuwa na haya ya kusema: “Leo hii nchini Tanzania,
mmjoa kati ya kila Wanawake wane chini ya umri wa miaka 19 wamekwisha kuwa
wazazi na asilimia 20% ya Wanawake chini ya umri wa miaka 20 wamo katika ndoa
za kulazimishwa.
Zaidi ya hayo, kama
binti akipata ujauzito hata kwa kubakwa, anafukuzwa shule na huo ndio unakuwa
mwisho wa elimu yake. Haya siyo mazingira mazuri ambayo vijana wetu wanahitaji
iwapo wana matumaini ya kukuza uchumi wa taifa letu na kuliweka kuwa katika
kipato cha kati (middle income). Wanawake wana uwezo mkubwa wa kuchangia kukua
kwa taifa letu, hivyo ni jukumu letu kuwapa fursa hizo”.
“Nina imani kubwa kuwa
tutafanikiwa”, aliongeza Lady Jaydee, “tunataka kila mmoja atambue kuwa ana
haki ya kuchagua muda na wakati wa kupata watoto, na pia idadi ya watoto
wanaowataka. Marie Stopes na taasisi nyingine zinaweza kukusaidia kumaliza
masomo yako na kuhakikisha kuwa una maliza elimu na kuwa na mwanzo mzuri wa
maisha, kabla hujaamua kuwa mzazi. Name nitaanza kueneza ujumbe huu Jumamosi
hii kwenya Nyama Choma Festival, Dar es Salaam!”
Tukio hili la Lady
Jaydee kutembelea Hospitali ya Marie Stopes jijini Dar es Salaam litaonyeshwa
jumapili tarehe 07 Septemba kwenye East Africa TV. Kituo hiki kilichopo Mwenge
ni miongoni mwa hospitali 11 za Marie Stopes nchini Tanzania. Zote hizi zinatoa
huduma za uzazi wa mpango kwa Wanawake bure kabisa bila malipo yoyote.
No comments:
Post a Comment