Tangazo

September 18, 2014

MSTAHIKI MEYA WA ILALA JERRY SILAA ASHUSHA NEEMA KWA SHULE YA MSINGI KIVULE‏‎

Meza kuu ikiwa imepambwa na viongozi mbalimbali kwaajili ya kupokea msaada wa madawati Meya wa manispaa ya  Ilala Jerry silaa akabidhi msaada wa madawati mia moja katika shule ya msingi kivule iliyopo jijini dar es salaam ikiwa ni mpango aliouanzisha na kuanza kuutekeleza kupitia (meya boll) katika mpango huo madawati hayo yamekabidhiwa kwa mwalimu mkuu wa shue hiyo pamoja na diwani wa kata ya kivule na afisa elimu wa manispaa ya ilala walikuwepo katika shuguli hiyo ya kupokea msaada huo Jana
 Bw.Nyansika G Motena ambaye ni Diwani wa kata ya kivule katika halmashauri ya ilala akiongea machache kumkaribisha mstahiki meya
 Mwalimu mkuu wa shule ya msingi kivule akisoma Risala ya shule hiyo kabla ya kukabidhiwa msaada wa madawati
 Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa akizungumza mara baada ya kupokea risala iliyo somwa na Mkuu wa shule ya kivule
 Mh.Akifurahi na wanafunzi wa shule hiyo ambapo walikuwa na furaha wa kupokea msaada huo
 Mstahiki Jerry Silaa meya wa Ilala akimkabidhi msaada huo wa madawati mia moja (100) mwalimu mkuu wa shule ya msingi kivule 
  Mstahiki Jerry Silaa meya wa Ilala akipeana mkono wa shukrani na mratibu Bw.Mkami Sudayi
 Diwani wa kata ya kivule Bw.Nyansika Motena akitoa shukrani kwa meya mara baada ya kukabidhiwa msaada huo
 Afisa elimu wa Ilala Bi. Bi Elizabeth Thomas naye pia aliungana na wenzake kuweza kumpa mkono meya wa ilala Jerry Silaa
 Waalimu wa shule ya kivule wa kiwa katika picha ya pamoja na Mh.Jerry Silaa mara baada ya kukabidhiwa madawati hayo
 Wanafunzi wakishangilia kwa furaha na meya  wakiwa wamekabidhiwa msaada huo wa dawati miamoja
 picha  Jerry Silaa meya wa Ilala akiwa na daadhi ya viongozi na wanafunzi 
  Afisa Elimu wa Manispaa ya Ilala, Bi Elizabeth Thomas akiongea maneno ya shukrani kwa meya mara baada ya shughuli ya kukabidhi kumalizika
 Mwanafunzi Frednand  chales akiongea maneno ya shukrani kwa meya mara baada ya shughuli ya kukabidhi kumalizika
 Kwenye picha ni baadhi ya madawati yaliyotolewa na Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa katika shule ya kivule iliyopo manispaa ya Ilaa jijini Dar es Salaam
 baadhi ya wanafunzi wakiwa wanaendelea kusikiliza tukio liendavyo
 Kikundi cha ngoma cha makirikiri kilichoundwa na wanafunzi kwaajiri ya kusherehesha katika sherehe hiyo ua kukabidhi madawati mkatika shule ya kivule
 Burudani ikiwa imepamba moto kwa kusherehesha wahudhuriaji  na kikundi hicho
 kauli iliyopo katika madawati hayo.
 
 kundi la burudani ka kikulwa likiwa linatoa burudani wakati wa kukabidhi madawati hayo
 Mh:Jerry Silaa akiwa ameongozana wa viongozi mbalimbali walio kuwepo katika shughuli hiyo kwenda kukagua madarasa mawili mapya yaliyo jengwa hivi karibuni 
 Akizungumza na viongozi hao mara baada ya kuangalia madarasa hayo ambayo nayo ameshirika katika kuchangia wakati wa ujenzi
Haya ndiyo madarasa ya vyumba viwili mapya yaliyo jengwa hivi karibuni katika  shule ya kivule.

Akikabidhi madawati hayo Mh. Jerry Silaa amewaasa kuwa hata yeye alikuwa anasoma na anakaa chini lakini kwa kizazi cha sasa yatupasa tubadilike hiyo hatapenda kuona watoto wakiendelea kukaa chini  na kusoma katika mazingira magumu kama aliyo weza kusoma yeye  kwahiyo kwa moyo wake anarudisha fadhira kwa watanzania  kwa kushirikiana na wadau mbal;imbali kwa misaada tofautitofauti katika kipindi chake cha uongozi kwa nafasi ya meya.

Aidha muheshimiwa aliweza kuwafafanulia baadhi ya watu walio weza kufika katika hafra ya kukabidhi madawati kwa shule ya kivule kwamba kodi za pango zinavyo kusanywa huwa haziliwi na mtu zaidi ya kutatua matatizo katika sehemu mbalimbali ya halmashauri kwahiyo aliwaomba watu wote wasiwe na imani ya kuliwa kwa fedha hizo bali watambue zinakazi nyingi na tofauti tofauti katika halmashauri husika.

Naye mwalimu mkuu wa shule ya kivule wakati akisoma risala waliyo iandaa kwaajiri ya shughuli hiyo alisema shule ya kivule inawanafunzi wengi ambao ni takribani ya wanafunzi 2020 ambapo inakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa madawati, matundu ya vyoo,nyumba za walimu ambapo kwa sasa kuna nyumba moja tu,waalimu wa masomo mbalimbali pamoja na vifaa vya kufundishia hususani  somo la Tehama,hivyo kupelekea waalimu kutumia nguvu katika ufundishaji.

Bw.kubilu Lupembe  Dede  ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya kivule ametoa shukrani za dhati kwa mstahiki meya  wa ilala Jerry Silaa ambapo ameonesha nia ya dhati katika kufanikisha elimu inasonga mbele kwa kujitoa sehemu mbalimbali  na kuwa karibu na jamii

Pia diwani wa kata ya kivule Bw.Nyansika.G.Motena ametoa shukrani kwa niaba ya wananchi wote kwa kile anacho kifanya mheshimiwa meya wa ilala Jerry Silaa ameweza kukifany ana kusema inapaswa kuwa kiongozi wa mfano kwa wengine  

No comments: