Mwanamuziki nguli nchini, King Kikii akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu
ushiriki wake katika onyesho la muziki lililoandaliwa na kitengo cha
huduma kwa wateja kupitia Mradi wa 'Tunakujali' kwa ajili ya
kukusanya pesa za kuchangia shule ya watoto wenye mahitaji maalum ya Pongwe
mkoani Tanga, litakalofanyika kesho Septemba 03, katika
viwanja vya Airtel Makao Makuu. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel
Tanzania, Jackson Mmbando (wa pili kulia), ni Mkurugenzi wa Huduma kwa
Wateja wa Airtel, Adriana LYamba na Mwanamuziki nyota, Banana Zorro.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es salaam
Airtel yaanzisha mradi wa huduma kwa jamii
ujulikanao kama TUNAKUJALIKampuni Airtel Tanzania leo imetangaza
kuanzisha mpango wa huduma kwa jamii utakaowashirikisha wafanyakazi
wake kujitolea na kushiriki katika kuchangia na kusaidia
jamiii nchini.
Mpango unategemea kuanza wiki hii unashirikisha
wafanyakazi kutoka katika vitengo mbalimbali utawawezesha
wafanyakazi hawa kuandaa shughuli zitakazowawezesha kukusanya fedha
kwaajili ya kusaidia shule mbalimbali ambazo zina mahitaji muhimu katika
maeneo mbalimbali nchini.
Mradi huu umezindulia rasmi na Kitengo cha
huduma kwa wateja ndio kitakuwa cha kwanza kushiriki ambapo wameandaa
burdani ya musiki itakayowashirikisha magwiji mahiri wa muziki
nchini King KiKii na Banana Zoro inayotegeme kufanyika siku ya
jumatano tarehe 3 septemba 2014 katika viwanja vya ofisi ya Airtel.
Wafanyakazi wa Airtel na watu mbalimbali kutoka nje wamealikwa kushiriki
na kiasi cha pesa kitakachopatikana kitaenda kuchangia shule ya
watoto wenye mahitaji maalum Tanga.
Akiongea kuhusu mpango huu Meneja Uhusiano wa
Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema” katika kushiriki kutatua
changamoto mbalimbali zinazozikumba jamii wafanyakazi wa Airtel
wameona ni muhimu kuanzisha mpango huu maalumu wa kusaidia jamii. Airtel
kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii umeonelea ni vyema kutenga siku
14 mahususi kwa wafanyakazi kupata muda wa kusaidia jamii. Hivyo
tutakuwa na shughuli mbalimbali kuanzia sasa zitakazofanya na
wafanyakazi katika kukusanya fedha na kisha kufatiwa na siku 14 za kutoa
misaada wa jamii zinazotegemea kuanza rasmi mwakani mwezi wa
tatu. Lengo letu ni kuhakikisha tunazifikia shule 10 na kuzisaidia
kwa sasa na leo tunachukua nafasi hii kuwaalika wafanyakazi wetu
na jamiii kutuunga mkono na kushirikiana nasi”.
“Baadhi ya shule zitakzofaidika na mpango huu ni
pamoja na shule ya Msingi Pongwe Tanga itakayojengewa darasa,
shule ya msingi ya kumbukumbu Dar es salaam itapatiwa msaada wa
viti na meza kwa darasa la watoto wa masomo ya awali, shule ya
sekondari Ndala watapewa vifaa vya ofisi kwa wafanyakazi , uhuru
mchanganyiko watanunuliwa mashine ya Braile pamoja na vifaa vya kufundishai
na shule ya msingi kimara watapatiwa tanki ya kuhifadhi maji.
Nia yetu ni kuhakikisha tunazifikia shule nyingi
zaidi na jamii kwa ujumla “aliongeza Mmbando.Airtel Tanzania
imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia sekta ya elimu nchini
mpaka sasa zaidi ya shule 1000 zimeweza kufaidika na vitabu kupitia mradi wa
Shule yetu” wiki iliyopita
Airtel imetangaza zaidi ya shule 30
zitakazofaidika na misaada ya vitabu kwa mwaka huu wa 2014 na leo kupitia
wafanyakazi wake Airtel inaendelea kuwafikia watu wengi zaida na jamii
nzima kwa ujumla nchini.
No comments:
Post a Comment