MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga raia wa Brazili Geilson Santana Santos 'Jaja aliwatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo baada ya kufunga bao pekee lililoipa ushindi timu yake wakati ilipopambana na Thika United ya Kenya leo kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kimataifa kwa Yanga inayo nolewa na kocha Mbrazili Marcio Maximo,ambayo katika mchezo huo ilionyesha kiwango cha kuvutia katika kipindi cha kwanza na kupoteza nafasi nyingi za magoli sawa na wapinzani wao Thika Unite ambayo ilikuwa ikicheza kwa kutegemea mashambulizi ya kustukiza zaidi.
Ushindi huo unaifanya Yanga iliyomaliza nafasi ya pili msimu uliopita kucheza mechi nne za kirafiki bila kupoteza hata mchezo mmoja baada ya awali kuzifunga timu za Chipukizi,KMKM na Shangani za Zanzibar ilipokuwa kwenye ziara ya siku 10 Visiwani humo.
No comments:
Post a Comment