Meneja Uhusiano wa Airte Bwana Jackson Mmbando
akiongea na wasanii chipukizi wa Kijiwe cha Matofali mkoani Morogoro wakati
Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano
ya Airtel Trace Mkoani humo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Wasanii chipukizi kutoka Morogoro watembelewa katika
vijiwe vyao na kujiunga na mashindano ya Airtel Trace
Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel
imeendelea kuwafikishia wateja wake na wapenzi wa muziki katika mikoa
mbalimbali na kuwaunganisha katika mashindano ya kutafuta mwamamuziki chipukizi
ya Airtel Trace yaliyozinduliwa rasmi nchini mwanoni mwa mwezi octoba. Airtel
imetembelea Mkoa wa Morogoro na kuzindua rasmi huduma ya Airtel Trace music
star katika vijiwe mbalimbali mkoani hapo.
Akizungumza na wasanii chipukizi wa
muziki wa kizazi kipya katika vijiwe mbalimbali mjini Morogoro, Meneja uhusiano
wa Airtel Jackson Mmbando amesema huduma hiyo inamuwezesha mtu yeyote mwenye
kipaji cha kuimba kujiunga na kushiriki kwa kupitia simu ya mkononi kwa
kupiga namba 0901002233 kisha kurekodi wimbo wake na kuutuma.
Mashindano haya yanatoa mwanya wa
watanzania wenye ndoto za kuwa wanamuziki nyota kupata fulsa ya kuzifikia ndoto
zao. Sambamba na hilo tutakuwa na washindi watakaojishindia zawadi mbalimbali
hapa nchini kama vile pesa taslimu na nafasi ya kushinda na kushiriki
mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini south Afrika na kushirikisha
washindi wengine toka nchi 13 barani afrika ambabo Mshindi wa Afrika atapata
nafasi ya nafasi kwenda kurekodi wimbo wake nchini Marekeni na kupata mafunzo
ya muziki kutoka kwa msanii nguli wa muziki Akon huko nchini Marekani.
Nao baadhi ya wasanii waliokutwa kwenye
vijiwe vyao waliweza kushiriki shindano hilo kwa kurekodi nyimbo zao kupitia
Airtel Trace muziki star huku wakiishukuru Airtel kwa kuwaletea huduma ambayo
itawakomboa wasanii chipukizi wasio na uwezo.
Ambapo Hamis Ramadhan aka brash
waya 2 alikuwa na haya ya kusema” tunashukuru Airtel kwa kutuletea mshindano
haya kitaani kwani tunavipaji lakini tunashindwa kupiga hatua kwakuwa uchumi ni
mdogo tunaamini kwa kuppitia Airtel Trace tutatoka , kukubwa ni kusaidia na
kupigiana kura ili tufanikiwe, tunaamini Airtel Trace Tanzania Atatokea
Morogoro na hivyo natoa wito kwa wanamorogoro wajiunge kwa wingi na kutumia
nafasi hii ili kubuka kuwa masuper star.
Kwa upande wake Ramadhani Nguyao alisema
“ nimefurahia mpango mkubwa na wakwanza Tanzania utakaowawezesha wasanii
chipukizi kupata fulsa ya kuimba na kurecord wasanii wakubwa kama Akon. Mimi
nimevutia na ntajiunga na mashindano haya na waomba watanzania wengi na
wasanii wenzangu wa Morogoro na nje ya Morogoro kujiunga na kushiriki katika
mashindano haya ya Airtel Trace Music Stars.
Mashindano ya Airtel Trace Music Stars
yalizinduliwa rasmi nchini Mwanzoni na October na yatadumu kwa muda wa mienzi
sita ambapo fainali ya mashindano haya inategemea kufanya Mwaka kesho Machi
2015 nchini South Afrika.
No comments:
Post a Comment