Garden Avenue in
Dar es Salaam will be renamed to Hamburg Avenue
On 30th October the Garden Avenue in Dar es Salaam City Center will be
renamed to Hamburg Avenue to reflect the town twinning between the two cities.
With this gesture the City of Dar es Salaam responds to the dedication of a
“Dar-es-Salaam-Platz” in Hamburg Harbour
City last year.
At 11.00 PM on Thursday, October 30th,
a grand opening with invited guests will be held on Garden Avenue in front of
the Ocean Road Hospital.
Following an invitation by Lord Mayor
Dr. Massaburi and the City Council a delegation from the City of Hamburg will
be present at the event. Among the delegation Dar es Salaam welcomes the State
Counsellor of Hamburg, Mr. Wolfgang Schmidt, and the Honorary Consul of
Tanzania in Hamburg, Mrs. Petra Hammelmann.
The partnership between
the two port cities Hamburg and Dar es Salaam was established in 2010 and has
been a success story from its first day. Over the past four years the two
port-cities have established a network of vivid exchanges and lively
cooperation.
The
renaming on Thursday is an important step to make the city-partnership even
better known in Dar es Salaam and win new supporters in all parts of the
population. Given that the partnership has only existed officially for four
years, the range of activities between the two cities is truly outstanding.
These includes amongst others:
-
Partnerships between seven schools in Hamburg and
schools in DareEs Salaam
-
A network of youth groups
-
Cooperation of universities (students organize
exchanges and spend a term studying abroad)
-
Partnership between parishes
-
Opportunities for experts from Dar es Salaam to use
professional training facilities in Hamburg
-
The sole Tanzanian Honorary Consul in Germany is based
in Hamburg.
-
Cooperation of the port authorities of Hamburg and Dar
es Salaam
-
friendship between the Music Mayday Music School in Dar Es Salaam and the
Hamburg School of Music
As part of the
network “50 Municipal Climate Partnerships” of the Service Agency Communities
in One World (SKEW) Hamburg and Dar es Salaam have developed a joint action
program. The two cities foster the sharing of knowledge between their local
authorities regarding climate change, infrastructure projects, emergency
management, public waste management systems etc..
In this
context a specialist of the International Centre for Migration and Development
(CIM), Mr. Benjamin Klaus, works at Dar es Salaam City Council as Integrated
Expert at Association of Local Authorities of Tanzania (ALAT), funded by the
German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development. He strives to
strengthen the local authorities, to foster the town twinning and to support
professional public waste management. Soon one more specialist from Germany
will support his efforts and strengthen the team at Dar City Council to help
establish a professional public waste management.
Shortly – and
as a premiere in Tanzania - compost
works will be established in Kinondoni funded by the Kinondoni Municipal
Council, the German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development
and the City of Hamburg.
A further
lively cornerstone of the friendship between the two cities is the “Week of
Partnership”, which is being held in Hamburg every year. In 2014 the event took
from 18th to 28th September 2014. Over 90 guests from Tanzania, among them
politicians and representatives of civil society, visited Hamburg and
experienced a week of successful networking.
BARABARA
YA GARDEN JIJINI DAR SASA KUITWA BARABARA YA HAMBURG
Tarehe 30 Oktoba Barabara ya Garden (Garden Avenue) katikati
ya Jiji la Dar Es Salaam itabadilishwa jina na kuwa Barabara ya Hamburg ili
kuakisi ushirikiano wa karibu kabisa baina ya majiji haya mawili.
Hatua hii ya Jiji la Dar Es Salaam ni kumbukumbu na pia
mwitikio wa heshima wa jina la Dar Es
Salaam-Platz, eneo lililopo katika Jiji
la Bandari la Hamburg, tukio lililofanyika mwaka jana.
Siku ya Alhamisi, tarehe 30 Oktoba, saa 5.00 asubuhi,
sherehe kubwa itakayohudhuriwa na wageni waalikwa itafanyika katika Barabara ya
Garden mbele ya Ocean Road Hospital.
Kufuatia mwaliko uliotolewa na Mstahiki Meya Dr. Didas
Massaburi na Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam, ujumbe kutoka Jiji la
Hamburg utahudhuria sherehe hiyo. Miongoni mwa watakaokuwamo katika ujumbe huo
ni pamoja na Diwani Mkuu wa Jimbo la Hamburg, Bw. Wolfgang Schmidt, na Balozi
wa Heshima anayeiwakilisha Tanzania Jijini Hamburg, Bibi Petra Hammelmann.
Ushirikiano baina ya majiji haya mawili ya bandari ya
Hamburg na Dar Es Salaam ulianzishwa mwaka 2010, na umekuwa na mafanikio tangu
siku yake ya kwanza. Katika kipindi cha miaka minne iliyopita majiji haya
mawili yameanzisha mtandao wa mabadilishano katika nyanja mbalimbali yaliyo
dhahiri na ushirikiano wa dhati.
Kubadilishwa huko kwa jina la barabara siku ya Alhamisi ni
hatua muhimu katika kuufanya ushirikiano huo ujulikane zaidi Jijini Dar Es
Salaam, na kupata watu watakaouunga mkono katika makundi yote ya jamii.
Kutokana na kwamba ushirikiano huo umekuwapo rasmi kwa miaka minne, mlolongo wa
shughuli baina ya majiji haya mawili kwa kweli umekuwa wa aina yake.
Hii inajumuisha pamoja na mambo mengine:
-
Ushirikiano baina ya shule saba jijini
Hamburg na shule za jijini Dar Es Salaam
-
Mtandao wa vikundi vya vijana
-
Ushirikiano wa vyuo vikuu (wanafunzi
hutayarisha ziara za kubadilishana na kutumia muhula mmoja wa mafunzo nchi za
ngàmbo)
-
Ushirikiano baina ya parokia mbalimbali
-
Fursa kwa wataalamu kutoka Dar Es
Salaam kutumia taasisi za mafunzo jijini Hamburg
-
Balozi pekee wa Heshima wa Tanzania
nchini Ujerumani yupo katika jiji la Hamburg
-
Ushirikiano wa mamlaka za bandari za
jiji la Hamburg na Dar Es Saalaam.
Kama sehemu ya mtandao
ujulikanao kama „50 Municipal Climate Partnerships“ wa Jumuiya za
Uwakala wa Huduma katika Dunia Moja (SKEW), majiji ya Hamburg na Dar Es Salaam
yameanzisha mpango mkakati wa pamoja. Majiji haya mawili yanaendeleza
ushirikiano wa maarifa baina ya mamlaka zao za mitaa kuhusu mabadiliko ya tabia
nchi, miradi ya miundo mbinu, menejimenti ya dharura, mifumo ya maji taka n.k.
Katika muktadha huu mtaalamu kutoka Kituo cha Kimataifa cha
Uhamaji na Maendeleo (CIM), Bw. Benjamin Klaus, anafanya kazi katika
Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam kama Mtaalamu katika Jumuiya ya Mamlaka za
Serikali za Mitaa nchini Tanzania (ALAT), inayogharamiwa na Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya
Ujerumani.
Anajitahidi kuimarisha
mamlaka za serikali za mitaa ili kuendeleza ushirikino kati ya majiji haya
mawili na kusaidia menejimenti ya maji taka. Hivi karibuni mtaalamu mwingine
zaidi kutoka Ujerumani atasaidia juhudi zake na kuimarisha uwepo wao katika
Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam ili kusaidia uanzishwaji wa menejimenti ya
maji taka.
Hivi karibuni – na kwa mara ya kwanza nchini Tanzania-
shughuli za utengenezaji mboji zitaanzishwa wilaya ya Kinondoni na kugharamiwa
na Halmashauri ya Baraza la Kinondoni, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na
Maendeleo ya Ujerumani na Jiji la Hamburg.
Msingi mwingine ulio dhahiri wa urafiki baina ya majiji haya
mawili ni „Wiki ya Ushirikiano“, ambayo hufanyika jijini Hamburg kila mwaka.
Mnamo mwaka 2014 shughuli hiyo ilifanyika kutoka tarehe 18 hadi 28 Septemba,
2014. Wageni zaidi ya 90 kutoka Tanzania, mingoni mwao wanasiasa na wawakilishi
wa vyama vya kiraia walizuru jiji la Hamburg na kushuhudia wiki ya ushirikiano
iliyokuwa na mafanikio.
No comments:
Post a Comment