Tangazo

March 27, 2017

Airtel yazindua maduka 15 mkoani Morogoro

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Maisha Maganga akiongea wakati wa uzinduzi wa duka la Airtel l lililopo maeneo ya stendi ya Msamvu mkoani Morogoro ambapo Airtel pia ilitangaa rasmi maduka 15 mapya ambayo yanatoa huduma katika maeneo mbalimbali mkoani hapo.
 XXXXXXXXXXXX

Morogoro,

KUFUATI kutangaza mpango wake wa kuzindua maduka zaidi ya 2000 nchi nzima,  kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua maduka 15 katika mkoa wa morogoro  kwa lengo la kuhakikisha bidhaa na huduma zake zinawafikia wateja wake kwa ukaribu na urahisi zaidi

Akiongea wakati wa uzinduzi , Meneja Mauzo kanda ya Morogoro, Albert Mtalemwa alisema “ leo tunazindua maduka 15 mojawapo likiwa hapa ndani ya kituo cha mabasi kilichopo Msavu Morogoro kwa  lengo la kuwawezesha   wasafiri na wale wanaoingia kutoka maeneo mbalimbali, wafanyabiashara na wakazi wa Morogoro wanaotembelea kituo hiki kupata huduma zetu za Airtel husasani huduma ya kifedha kupitia simu za mkononi kwa urahisi zaidi na wakati wowote.

Maduka mengi ya Airtel ambayo yanafanya kazi ya kutoa huduma yapo katika maeneo mbalimbali ambayo ni pamoja na Itigi, Gairo,Kilombero na,mjini, Kilosa karibu na kituo cha mabasi, Kimamba mjini, Ruaha, Dumila, Dakawa karibu na soko, Mikese karibu na mizani,  kituo cha Kisaki,  Soko la Bwawani, Ifakara mjini  na  Ifakara kituo cha basi.

Lengo letu ni  kuziweka huduma zetu karibu na wateja wetu ili  kutatua changamoto zao za mawasiliano kwa wakati na kuwawezesha kupata huduma za kifedha kwa urahisi. Tunaamini maduka haya yataongeza idadi ya vituo vyetu na kuboresha kiwango katika huduma zetu”. aliongeza Mtalemwa

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, , Maisha Maganga alisema”  nawapongeza sana Airtel kwa mpango huu unaochochea kuboresha huduma zake kwa wateja lakini pia kuhakikisha usalama katika huduma za kifedha kupitia maduka haya. 

Hii ni fursa pekee kwa kwa wenye maduka kushirikiana na Airtel na kuongeza mitaji yao lakini pia tunaamini kupitia maduka haya yataongeza  ajira kwa vijana na kuboresha usalama wakazi na pesa zao kwani sasa wakazi wa maeneo ya hapa yatatunza pesa zao kwenye simu na kuzitoa kwa urahisi kupitia maduka haya.

Uzinduzi wa maduka ya Morogoro umefatiwa na uzinduzi wa maduka 8  mkoani Shinyanga wiki iliyopita na huku mpango wake mzima ni kuwa na maduka mengine kama hayo ya 2000 nchi nzima.


No comments: