Tangazo

October 2, 2014

KAMPENI YA HAKI YA UCHUMI KATIKA MASWALA YA KILIMO YAENDESHA MDAHALO WA KUHAMASISHA WAKULIMA WADOGO WADOGO HUSUSANI WANAWAKE


 Meneja wa Kampeni haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akifungua Mdahalo huo na mafunzo juu ya Kujenga hoja ya upatikanaji wa Chakula na haki ya chakula, Kufuatilia upatikanaji wa haki kwenye Rasilimali za Ardhi na matumizi yake,na kuhamasisha uwekezaji kwa wakilima wadogo wadogo Hususani wanawake kwenye Muktadha wa mabadiliko ya Tabia nchi, katika kampeni ya GROW 
 
Mmoja wa washiriki wa Semina hiyo akielezea matarajio yake akiwa kama Mama shujaa wa Chakula na Mkulima mwanamke Jinsi ambavyo wameweza kusaidiwa na Oxfam kufikia malengo yao katika kilimo na kuwa wakulima Bora wenye mfano wa Kuigwa
Mshindi wa Maisha Plus 2012 Bernick Kimiro akitoa mchango wake Jinsi kilimo kinavyo weza kumsaidia mwanamke na kufikia Malengo yake.
Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula 2014 , akiendelea kuchukua Maoni mbalimbali , Mchango na mawazo ya watu mbalimbali katika Mdahalo huo.
Oscar Munga kutoka Forum CC akitoa ufafanuzi wa kina juu ya mahusiano ya kilimo na mabadiliko ya Tabianchi, Pia alizungumzia ni namna gani watu wanaweza kujikomboka katika kilimo na kuendana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Balozi wa Oxfam kupitia kampeni ya GROW Khadija Mwanamboka akielezea umuhimu wa kilimo bora na uwezeshaji wa wanawake katika kupata haki za Ardhi lakini pia jinsi gani Mwanamke anaweza kujikomboa katika kilimo na kuwa wanawake wanahaki sawa katika swala zima la kumiliki Ardhi.
Wa kwanza kulia ni mmoja wa aliyekuwa mshiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 kutoka Zanzibar akitoa Mchango wake kuhusu Umiliki wa Ardhi na kuelezea jinsi gani wanawake wasivyo na haki ya Ardhi hiyo, na kuomba kwamba nao ni binadamu na wanahaki sawa ya kumiliki ardhi hiyo
Wakili Joseph Chiobola ambaye ni Afisa Programu kutoka Haki Ardhi akitoa ufafanuzi wa kina juu ya haki za watu kumiliki Ardhi, pia alieleza kwa kina sababu za watu mbalimbali kugombania Ardhi na kueleza namna gani Migogoro ya Ardhi inatokea na Njia za kuimaliza Migogoro hiyo.
Mkamiti Mgawe kutoka Oxfam Akichangia Jambo katika Mdahalo huo
Afisa Ushawishi wa Ardhi kutoka Oxfam Naomi Shadrack akiendelea kutoa muongozo katika mdahalo huo.
Mchoraji Maarufu wa Katuni Muhidini Msamba akitoa mchango wake juu ya mada ambayo ilikuwa inahusu mazao kuto kuwa na thamani kuwa ndio moja ya chanzo cha wakulima waliowengi kutoka Tanzania kukosa  Masoko katika mazao yao, aliongeza ushauri kuwa kunahitajika nguvu ya ziada ili kujikwamua katika swala hilo kwa ujumla
 Mama Shujaa wa Chakula 2012 akitoa ushuhuda wake jinsi Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Oxfam Jinsi walivyo weza kumpa Shamba ambalo mpaka sasa Linamsaidia yeye pia watu wengine kupitia elimu anayoitoa ya Shamba Darasa kwa wakazi wa eneo analoishi huko Morogoro. na kusisitiza kuwa na matumizi Bora ya Ardhi.
 Mmoja wa Washiriki Akichangia Mada juu ya rushwa kuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa wakulima na kuwa kuna Baadhi yao wanamazao mazuri lakini kutokana na kuwa mkulima mdogo anashindwa kuuza mazao yake na badala yake anayeuza mazao hayo ni Mkulima mkubwa ambaye huweza kutoa hongo na Mazao yake kununuliwa kirahisi
Mshindi wa Shindano la Maisha Plus 2014 Boniface akitoa maelezo na kuchangia katika Mdahalo huo
Tajiel Urioh kutoka Forum CC akihitimisha Mdahalo huo
Washiriki wakiendelea kufuatilia kwa makini Mdahalo huo
 Kila mmoja akiwa makini kuhakikisha anapata Somo na kulielewa ili apate kwenda wafundisha na wengine.
 Washiriki wakiwa katika Mdahalo huo

No comments: