Tangazo

October 2, 2014

KINANA AUNGURUMA PANGANI TANGA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mwera, wilayani Pangani, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010 mkoani Tanga.Kinana ameziagiza wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutatua haraka migogoro ya ardhi nchini. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Sehemu ya umati wa wananchi ukiwa kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Kinana
 Kinana akilakiwa na wananchi katika Kiji cha Mkalamo, wilayani Pangani ambapo alizindua mradi wa maji.
 Wanananchi wa Kata ya Mkaramo wakipata huduma katika kisima kipya cha maji kilichozinduliwa na Kinana.
 Kinana akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa kisima cha maji katika Kata ya Mkaramo, wilayani Pangani
 Kinana akifungua maji kwenye bomba wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji katika Kata ya Mkaramo
 Kinana akizungumza jambo na mama baada ya kumtwisha ndoo ya maji wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji katika Kata ya Mkaramo
 Kinana akishiriki kuchimba mtaro wa kuweka mabomba wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji
 Watoto wakichangamkia kuteka maji katika kisima hicho
 Kinana akibeba tofali baada ya kufyatua aliposhiriki ujenzi wa tawi la CC, Kata ya Mkwaja, Pangani
 Popooo zikiwa zimeanikwa ambapo Kinana alishiriki kubangua katika Kijiji cha Mseko, KKata ya Bungaa, wilayani Pangani.
Kinana akishiriki kubangua popoo katika Kijiji cha Mseko, wilayani Pangani.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aqkishiriki kubangua popoo katika Kijiji cha Mseko, wilayani Pangani, Tanga.
WanaCCM wakitumbuiza kwa nyimbo wakati Kinana alipowasili katika Kijiji cha Mseko, kushiriki ujenzi wa jengo la Tawi la Mseko, Kata ya Bumbaa
Kinana akishiriki kuweka dirisha katika jengo la CCM Mseko
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mwera, wilayani Pangani
Mbunge wa Jimbo la Pangani, Salehe Pamba akielezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa jimboni humo kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mwera, wilayani Pangani

No comments: