Tangazo

October 1, 2014

MAJAJI WAENDESHA MAHAKAMA YA WAZI KUSIKILIZA NA KUPOKEA MALALAMIKO YA WAKULIMA WALIONYANG'ANYWA ARDHI,WAFUGAJI NA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Jaji Mh. Richard Mziray Akitoa Hukumu katika Mahakama ya wazi  katika Kesi zote Mbili ya Kiteto na Kilosa ,ambapo katika Kesi ya Wilaya ya Kiteto alitoa Maamuzi kwamba kulikuwa na umuhimu wa utekelezeji wa Amri ya Mahakama na kuheshimu Amri za Mahakama kuwa Mahakama ilisha tamka kuwa ile ni Hifadhi hivyo inatakiwa kulindwa na kuheshimiwa na ameongeza kuwa kama kungekuwa na kuzingatiwa kwa Sera za Ardhi basi kusingekuwa na Migogoro yote hiyo ametolea mfano pia maeneo ambayo yanatakiwa kulindwa ni pamoja na Bahari na Hifadhi.Katika kesi ya Kiteto alimalizia kuwa Maamuzi ya Mahakama yangeheshimiwa basi kungekuwa hakuna hii Migogoro yote.

Katika Kesi ya Kilosa Mh. Jaji Richard alisema kwamba Mgogoro uliopo ni juu ya Maji katika Mto wa Mkondoa na Muyombo ambao unagombaniwa wa wafugaji pamoja na wakulima na kwamba katika mgogolo huu Serikali inapendelea zaidi Wakulima na kuwaacha wafugaji alisema kwamba ikiwa wafugaji wangekuwa wanasababisha uharibifu wa Mazingira basi wasinge Ruhusiwa kutumia mito hiyo na hakuna sehemu inaonesha wafugaji wanaharibu Mazingira. Hivyo wafugaji wanahaki ya kutumia mto huo.

Mwisho katika kesi zote Mbili Mh. Jaji  Richard Mziray alitoa Tamko lifuatalo kuwa Wafugaji wanahaki sawa ya kutumia mito hiyo, pia wafugaji wanahaki ya kushiriki katika maamuzi ya wakulima , Wanao lazimisha mkondo wa mito hiyo uende sehemu ambayo sio yake hawana mamlaka ya kufanya hivyo Mwisho ameshauri kwamba ili migogoro hii isiweze kuendelea kuna umuhimu wa upendo kwanza Baina ya pande zote Mbili wakilima na Wafugaji, wakifanya hivyo kutakuwa hakuna migogoro kulipo kungoja Amri za Mahakama.
 Majaji wakiwa wanasikiliza Kesi kwa Makini juu ya migogoro ya Ardhi na wafugaji, Wawekezaji wanachukua maeneo ya wanavijiji, Unyang'anyi wa ardhi na Mazingira kwa ujumla  Kutoka kushoto ni Mh. Jaji msaidizi Jonas, wa katikati ni Mh. Jaji Richard Mziray, na Mh.Jaji Msaidizi Emma Lukumai
 Muwezeshaji wa Mkutano huu Jenerali Ulimwengu akiendelea kutoa Mwongozo
Mlalamikaji wa Kesi ya matukio makubwa katika hifadhi za Murtangos na Sulendo Wilayani Kiteto Bwana Lembulu Ole Kosyamlos  kushoto akitoma malalamiko juu ya hifadhi ya E-Murtangos iliyoundwa na vijiji saba ambavyo ni Kimana,Ndirkishi, Emarti,Nhati, Engusero,O-sidan na Loltepesi ambapo walianza mchakato huo mwaka 1996 na kurasimishwa rasmi Mwaka 2002 na hifadhi hiyo inaukubwa wa Hekta za Mraba 133,33.15, alieleza changamoto za wafugaji na wakulima ambapo watu wengi walipoteza maisha,Wavamizi kuingia bila utaratibu na kuharibu mazingira, na wimbi la uvamizi kuendelea siku hadi siku mpaka kufikia mwaka 2013. 

Pia katika Mashitaka hayo ameiomba mahakama ya wazi iwasaidie kutatua tatizo lao na Serikali iangalie upya eneo hilo Kisheria na zisiingizwe Sheria katika Jambo Hilo.
Mh. Diwani lairumbe Mollel ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto akitoa Malalamiko yao Mbele ya Mahakama ya wazi juu ya Hifadhi ya Msitu wa Vijiji Lusendo ambapo alieleza kuwa hifadhi hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 1994/1995 ambapo vijiji 9 viliungana na kutengeneza hifadhi hiyo aliongeza baada ya kuanzisha hifadhi hiyo walipata mafanikio ikiwa ni pamoja na kujipatia fedha kupitia uvunaji wa miti , mkaa endelevu na asali , pia walifanikiwa kupata Gari moja aina ya Land Cruzer Pick up na pikipiki . 

Alimalizia kwa kuleta malalamiko yake katika Mahakama ya wazi kuwa kuna uvamizi uliokithiri kwa maeneo ya Misitu Hususani Maeneo yote yanayozunguka mipaka ya Wilaya za Kilindi na Kiteto na Kuiomba Serikari wapate kurejeshewa maeneo yao.
Bwana Henry Parmeo akitoa mashitaka yake Mbele ya Mahakama ya wazi  juu ya mgogolo uliopo Kilosa kati ya wafugaji na wakulima hasa katika eneo la maji, na muwekezaji ambaye yeye amebadilisha Mkondo wa Maji kutoka katika eneo lake husika na kwenda katika Mashamba, Katika kesi hiyo amedai kwamba wakulima wamekuwa wakiwalaumu wafugaji hao kuwa ndio wenye makosa kwa kuwa wanaingilia wakulima kuwa Mifugo yao inakula mazao na kusahau kwamba Wakulima hao wamebadilisha mkondo huo kwenda mashambani, na aliongeza kuwa mgogoro huu huwa unajitokeza hasa wakati wa kiangazi miezi ya Nane,Tisa, Kumi, Kumi na moja na Kumi na Mbili katika mto Mkondoa na Myumbo. ameiomba Mahakama ya wazi pamoja na Serikali kumaliza Mgogoro huu.
Mama Shujaa wa  Chakula kutoka Mkoa wa Morogoro akielezea kwa kina zaidi juu ya Mgogoro wa wakulima na wafugaji hasa katika mito miwili ambapo wote wanagombania kupata maji hasa wakati wa kiangazi na amewapongeza Oxfam kwa Juhudi zao za kusaidia kutatua matatizo ya Mgogoro huo
Bi Vera F. Mugittu Mjumbe wa Bodi ya Forum CC akitoa maelezo ya kina zaidi Juu ya Kesi Mbili zilizotajwa Kesi ya Kilosa na Kiteto na kusema kuwa Migogoro yote ni Juu ya Lasilimali na kwamba Serikali pamoja na Mahakama wanatakiwa kujua Matatizo haya na kujua Jinsi gani wanaweza kuyatatua na kuwajengea uwezo watu wapate kujitambua ili kuepukana na migogoro hiyo, Alimalizia kwa kusema kuwa ucheleweshaji wa kusikiliza kesi ndio unao ongezea Migogoro.
Bwana Muro Mjumbe wa Bodi ya Forum CC akitoa maelezo ya kina juu ya kesi mbili za Kilosa na Kiteto
Baadhi ya Wachangiaji wakichangia Michango na mawazo mbalimbali wakati wa Mahakama ya Wazi iliyo andaliwa na Oxfam pamoja na Forum CC
Mh. Emma akitoa ufafanuzi juu ya Vifungu mbalimbali vya Sheria wakati wa Hukumu hizo katika mahakama ya wazi leo
Mh.  Jonas akitoa ufafanuzi zaidi wa maamuzi katika kesi hiyo ya Mahakama ya wazi
 Michoro ambayo inaonesha matukio mbalimbali ya Mkutano huo
 Burudani ikiendelea wakati wa mapumziko mafupi
Baadhi ya watu wakiwa wanasikiliza kesi kwa makini katika Mahakama hiyo ya wazi ambayo iliandaliwa na Oxfam na Forum CC

No comments: