Tangazo

October 1, 2014

NSSF YATOA FURSA KWA WAKAZI WA MBEYA NA SONGEA

Kupitia Semina za Fursa zinazoendelea kufanyika katika mikoa mbali mbali hapa nchini, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imekuwa ikitoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi na kuwahamasisha kujiunga na mfuko huo ili waweze kunufaika na mafao ya NSSF hususani matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi wake pamoja na mikopo kupitia SACCOS.

Fursa nyingine kutoka NSSF ambazo mwanachama anaweza kunufaika nazo ni pamoja na Pensheni ya uzeeni, Pensheni ya Ulemavu, Pensheni ya Urithi, msaada wa Mazishi, Mafao ya Uzazi, mafao ya Kuumia Kazini.

Semina hizi zinatoa fursa kwa wajasiriamali, wakulima pamoja na watu mbalimbali waliojiajiri wenyewe na kuuliza maswali mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na NSSF na wengi hujiuga na NSSF baada ya kuona faida zake.

"Katika semina za Fursa NSSF inafanya uandikishaji wa wanachama wapya na pia inatoa nafasi kwa wananchi kuuliza na kufahamu mambo mbali mbali yanayohusu mfuko huo" alisema Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba.

Mpaka sasa NSSF imeshiriki katika Semina ya Fursa  katika mikoa ya Geita, Ruvuma, Mbeya na Morogoro. 
 Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba akitoa mada katika semina ya Fursa kuhusu Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi na kuwahamasisha wajiunge na mfuko huo ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa na NSSF hususani Matibabu Bure kwa mwanachama na wategemezi wake pamoja na mikopo kwa wanachama kupitia Saccos. Semina hiyo ilifanyika mkoani Mbeya hivi karibuni.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba (katikati), Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba (wa tatu kutoka kulia) wakiwa meza Kuu pamoja na wageni wengine wakati wa Semina ya Fursa iliyofanyika mkoani Mbeya.
 Baadhi ya umati wa wakazi wa Mbeya mjini wakifuatilia kwa makini Semina ya Fursa iliyofanyika katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa mjini Mbeya.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba akitoa mada katika semina ya Fursa Mbeya iliyodhaminiwa na NSSF kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi wakazi wa Mbeya.
Afisa Matekelezo wa NSSF, Ally Mkulemba akitoa mada kuhusu faida za kujiunga na NSSF kwa wakazi wa mjini Songea wakati wa Semina ya Fursa iliyofanyika mkoani Ruvuma.
Msanii wa Bongo Fleva Mwasiti Almasi akiwasihi wakazi wa Songea wajiunge na NSSF ili waweze kupata Fursa ya kujikwamua kimaisha kupitia mafao mbali mbali ya NSSF kama Mikopo kupitia Saccos, Matibabu Bure, Pensheni ya uzeeni, pensheni ya ulemavu, pensheni ya urithi, msaada wa mazishi, mafao ya uzazi, mafao ya kuumia kazini. 
Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba (kushoto) wakifuatilia kwa makini semina ya Fursa iliyofanyika Songea mkoani Ruvuma.

No comments: