Tangazo

October 4, 2014

WAFANYAKAZI WA UNFPA, TUSHIKAME PAMOJA FOUNDATION NA PROJECKT INSPIRE WAONYESHA UPENDO KWA WAZEE MSIMBAZI CENTRE

IMG_2450
Daktari kijana Brian Mushi wa Projeckt Inspire akionyesha upendo kwa mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho kilichopo Msimbazi Centre mara baada ya kumpima Presha wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.

Na Mwandisi wetu

WAZEE wanaoshi katika makazi ya Msimbazi Centre Jijini Dar es salaam karibu na kanisa la Mtakatifu Maria wa Fatma, Msimbazi walipata faraja kubwa baada ya kutembelewa na makundi matatu ya jamii
Makundi hayo ni pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini, Tushikamane Pamoja Foundation na madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy.

Makundi hayo yalifika katika kituo hicho katika kuadhimisha siku ya wazee duniani.

Wakiwa na lengo kuu la kuwafariji, kukagua afya zao na kuheshimu uwepo wao, makundi hayo pia yaliwapa zawadi za vyandarua, sabuni za kufulia na kuogea, pampers, Thermos Flask, vikombe vya chai, sahani za kulia, vijiko, sukari, njugu mawe, Tshirts, viatu, nguo, vyombo vya kufanyia usafi .

Pia walipiga picha za pamoja za ukumbusho.

Siku ya Wazee Duniani imetengwa kwa ajili ya kuweaenzi na pia kuwakumbuka kwa mambo waliyofanya kuendeleza kizazi cha wanadamu.
IMG_2514
Dr. Brian Mushi wa Projeckt Inspire akimpima presha mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho.
IMG_2523
Dr. Brian Mushi wa Projeckt Inspire akichukua vipimo vya damu kwa ajili ya kupima sukari kwa mmoja wa wazee wanaolelewa kwenye kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
IMG_2330
Wafanyakazi wa UNFPA kutoka kushoto ni Clementina Njau, Mike Mwakuvila na mdau kutoka Tushikamane Pamoja Foundation wakionyesha upendo kwa mmoja wa wazeee wanaoishi kwenye kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
IMG_2351
Dr. Majaliwa Marwa kutoka UNFPA akikabidhi moja ya vyandarua walivyovitoa kwenye kituo hicho kinacholelea wazee Msimbazi Centre wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
IMG_2383
Sehemu ya msaada uliotolewa na makundi hayo.
IMG_2371
IMG_2364
Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini wakiongozwa na mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza(kushoto), wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation pamoja madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy wakiwa kwenye picha ya pamoja na masista wanaowahudumia wazee hao kwenye kituo hicho.
IMG_2574
Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini wakiongozwa na mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza(wa nne kushoto), wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation pamoja madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy kwenye picha ya pamoja.
IMG_2579
Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini, wadau wa Tushikamane Pamoja Foundation pamoja madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy kwenye picha ya pamoja na mmoja wa wazee wanaoishi kituoni hapo.

No comments: