Tangazo

November 6, 2014

MFUKO WA GEPF WAPANUA WIGO KWA KUZINDUA OFISI MPYA NYANDA ZA JUU KUSINI MKOANI MBEYA

 Meneja wa kanda ya Nyanda za juu kusini Bw Ramadhan Sosora akitoa neno la ufunguzi na utambulisho kwa wanahabari.
 Meneja Masoko kutoka Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF Bw Aloyce Ntukamazina akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo kulia kwake ni Afisa masoko katika ofisi ya mbeya Bw Alex William.
 Pichani baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa makini maelezo wakati wa uzinduzi huo.
 Bw Aloyce Ntukamazina akielezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 toka 2004 – 2014 yaliyopelekea uzinduzi wa ofisi mpya nyanda za juu kusini.
  Uongozi wa Mfuko wa GEPF ukipokea maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari juu ya mipango ya Mfuko wa GEPF katika kupanua wigo zaidi na kufikia watanzania walio wengi.

Baadhi ya waandishi wa habari walioalikwa wakichukua picha za tukio hilo katika ukumbi wa mikutano wa Mfuko wa GEPF.

Bw Aloyce Ntukamazina Meneja Masoko wa Mfuko wa GEPF alielezea kuwa sababu kubwa zilipelekea kuzindua ofisi mpya nyanda za juu kusini kwanza ni ukuaji wa kasi wa shughuli za kiuchumi na kibiashara katika mkoa wa Mbeya lakini pia ni mafanikio makubwa ambayo Mfuko umeyapata kwa kipindi cha miaka 10 kutoka 2004 ambapo mfuko ulipata menejimenti yake rasmi hadi 2014.

Alisema Mfuko umekuwa katika vigezo vyote kwa upande wa wanachama wameongezeka kutoka 16,131 hadi kufikia 76,000, Michango imeongezeka kutoka TZS 5.1 Billioni kwa mwaka hadi TZS 37.29 Billioni na Thamani ya Mfuko imeongezeka kutoka TZS 20.21 Billioni 2004 hadi TZS 245.38 Billioni 2014.

Ukuaji huu umeonyesha Mfuko una afya njema na unaweza sasa kupanua wigo na kufungua ofisi mpya katika mikoa mingine.  Jambo la pili Bw Ntukamazina alieleza ni ukuaji wa kasi wa mpango wa hiari wa VSRS ambao kwa kipindi kifupi cha miaka mine tangu uanzishwe 2010 umeweza kuwasajili jumla ya wajasiriamali 35,481 ambao kwa kipindi kifupi hicho wamejiwekea akiba ya zaidi ya TZS 5.01 Billioni.  Alisema hii imedhihirisha kwamba mpango huu ni mkombozi kwa watanzania wote na Mfuko ukaona ni vyema sasa usogeze huduma zake karibu kwa watanzania waishio nyanda za juu kusini ili nao waweze kufaidika na mafao yatolewayo.


Mwisho Bw Ntukamazina alitoa wito kwa watanzania wote wajenge utamaduni wa kujiwekea akiba kwani uzee hauepukiki na ipo siku kila mmoja wetu ataishiwa nguvu za kuzalisha mali, lakini pia alisema GEPF kupitia mpango wa VSRS ina mipango madhubuti kuhakikisha kila mtanzania awe mkulima, mama lishe, mjasiriamali, muuza mitumba, mvuvi n.k nao wanalipwa Pensheni kama wengine walio katika ajira rasmi.

No comments: