Tangazo

November 12, 2014

WIKI YA UJASIRIAMALI TANZANIA KUANZA NOVEMBA 17

Mratibu wa Wiki ya Ujasiriamali Tanzania, Lilian Secelela Madeje (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maandalizi ya wiki hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 17 mwaka huu jijini humo. Kutoka kushoto ni mmoja wa wajasiriamali, Mboni Masimba wa kipindi cha Mboni Show na  Meneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Magabe Kibiti Maasa.
Meneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Magabe Kibiti Maasa (kushoto) akizungumza kuhusu kushiriki kwa DSE katika maadhimisho ya Wiki ya Ujasiriamali Tanzania yanayotarajiwa kuanza Jumatatu ijayo jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto kwake, ni Mratibu wa Wiki ya Ujasiriamali Tanzania, Lilian Secelela Madeje ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Professional Approach Development na Meneja Mradi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Rukia Lukanza.
Mmoja wa waanzilishi wa asasi ya KINU,   Emanuel Feruzi (kulia) akizungumza kuhusu ushiriki wao katika maadhimisho ya Wiki ya Ujasiriamali Tanzania. Kulia kwake ni Rukia Lukanza wa ILO na mratibu wa wiki hiyo, Lilian Secelela Madeje.
Mmoja wa wajasiriamali, Mboni Masimba  (kushoto),  wa kipindi cha Mboni Show anayetarajiwa kuwa mmoja wa watoa mada katika semina na mikutano wakati wa Wiki ya Ujasiriamali Tanzania akizumguza katika hafla hiyo. Kushoto kwake ni Meneja Miradi na Biashara wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Magabe Kibiti Maasa na mratibu wa wiki hiyo, Lilian Secelela Madeje.
Baadhi ya waratibu, wadhamini na waandishi wa habari wakiwa katika hafla ya utambulisho wa maadhimisho ya tatu ya Wiki ya Ujasiriamali Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

No comments: