Mratibu wa mbio za uhurumarathon 2014 Innocent Melleck katikati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya maandalizi yam
bio hizo kwa mwaka huu ambapo zitafanyika 07/12/2014 na kuongozwa na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete huku Zaidi ya wanariadha elfu kumi na tano kukadiriwa
kushiriki kwa mara ya kwanza.Kulia kwake ni Katibu mkuu wa shirikisho la riadha
nchini Selemani Nyambui na kushoto ni mjumbe wa chama cha riadha mkowa wa Dar
Es Salaam Tullo Chambo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya wanariadha 15,000 kutoka ndani na nje wanatarajiwa
kuthibitisha kushiriki katika mbio za Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa
kufanyika Desemba 7 kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini, Mratibu wa mbio hizo, Innocent
Melleck, alisema kuwa maandalizi yako katika hatua za mwisho huku akimtaja Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuongoa
mbio hizo.
Melleck pia jana alikabidhi ada ya Sh. Milioni mbili kwa
Chama cha Raidha Tanzania (RT) na Sh. Milioni moja kwa wenyeji Chama cha Raidha
Mkoa wa Dar es Salaam (DAAA), ili kupata kibali cha kuendesha mbio hizo.
Mratibu huyo alisema kuwa fomu kwa ajili ya kushiriki mbio
hizo zimeanza kutolewa jana na jijini zinapatikana katika maduka yote ya TSN,
huku pia zikitolewa kwenye mikoa ya Arusha, Moshi mkoani Kilimanjaro na
Leaders.
“Tunawashukuru wadau wote walioshiriki katika kujiandaa
kushiriki mbio hizo hasa klabu za jogging ambazo zinahamasisha wanariadha
kushiriki mbio hizo zenye kuhamasisha Amani, ushirikiano na mshikamano,”
alisema Melleck.
Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, alisema kuwa chama
kimeialika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, nchi za Afrika Mashariki na
mataifa mengine ambayo yako tayari kushiriki mbio hizo zitakazofanyika sambamba
na sherehe za Uhuru wa Tanzania.
Nyambui alisema kuwa wanariadha wamejiandaa kuonyesha vipaji
vyao na wanaamini yataendelea kukuza vipaji vyao kulitangaza jina la Tanzania.
Naye Mjumbe wa DAAA, Tullo Chambo, alisema kwamba chama
kimeshiriki kuanzia hatua ya awali na wanawahakikishia wadau kuwa mbio za mwaka
huu zitakuwa na mafanikio.
Chambo alisema kuwa wanazipongeza klabu na makundi yote
yanayoendelea kujiandaa kushiriki mbio hizo na kila kitu kitafanyika kwa
kufuata taratibu za kiufundi.
Melleck alitoa rai kwa makampuni na mashirika pia watu binafsi
kujitokeza kwa wingi ili kuweza kudhamini mbio hizi kwani bado nafasi ipo kwa
wale wote wenye nia ya kudhamini kwa mwaka huu
Mbio za Uhurumarathon kwa mwaka huu zinadhaminiwa na Kampuni
ya Bia nchini TBL kupitia kinywaji chake Grandmalt,Maji ya Uhui,Azam Tv,Tbc
1,Mwananchi Communications Ltd,Magazeti ya Uhuru,Jambo Leo,Michuzi
media,CxC Africa,Kitwe General
Traders,Samsung,Cokacola, Tindwa Mediacal Service,Gazeti la TABIBU,Konyagi,na
TSN SUPERMARKETS.
No comments:
Post a Comment