Tangazo

November 17, 2014

ZIARA YA KINANA KATIKA JIMBO LA MCHINGA LINDI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mchinga Ndugu Said Mtanda wakati wa mapokezi yake yaliyofanyika Kitomanga  Mkwajuni jimboni hapo wilaya ya Lindi vijijini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa jimbo la Mchinga waliojitokeza kumpokea.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza wimbo maalum wa mapokezi kutoka kikundi cha uhamasishaji cha CCM Mchinga mara baada ya kuwasili Kitomanga Mkwajuni jimbo la Mchinga.
 Katibu Mkuu wa CCM akishiriki ujenzi wa ghala la kijiji ambalo litatumika kuhifadhia chakula kwa wakazi wa Kitomanga Mkwajuni
 Wananchi wa kijiji cha Namkongo wakimpokea Katibu mkuu wa CCM kwa namna yake mara baada ya kuwasili kijijini hapo ambapo alizindua mradi wa maji na kukabidhi saruji kwa ajili ya ujenzi wa soko.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mbunge wa Jimbo la Mchinga  Ndugu Said Mtanda  namna wananchi wa kijiji cha Namkongo walivyopata tabu ya kutafuta maji
 Wananchi wa Namkongo walipata shida ya kutafuta maji hii picha inaonyesha aina ya visima ambavyo wananchi walitegemea kupata maji.
 Mbunge wa Mchinga  Ndugu Said Mtanda akisoma taarifa ya mradi wa maji kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Kila mtu wa kijiji cha Namkongo alikuwa na shauku ya kumuona Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mbunge wa Mchinga Said Mtanda akishiriki kuimba kwaya ya Kikundi cha Changamoto wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana  katika jimbo la Namkongo
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi saruji kwa ajili ya kusakafia soko.
 Katibu Mkuu wa CCM akifungulia maji kama ishara ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Namkongo.
 Mbunge wa Jimbo la Mchinga akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa Namkongo
 Katibu mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha maji Bi.Rehema Anafi mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika  kijiji cha Namkongo wilaya ya Lindi Vijijini.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinunua kashata kwenye soko la kijiji cha Namkongo, wengine pichani ni Mkuu wa wilaya ya Lindi vijijini Dkt. Hemid Nassoro (kulia),Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mbunge wa jimbo la Mchinga Ndugu Said Mtanda (kushoto).
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kukagua tenk la maji kijijini Namkongo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini mbunge wa Jimbo la Mchinga Ndugu Said Mtanda wakati wa mkutano na wananchi wa Kilangala.
 Katibu mkuu akipitia taarifa mbali mbali za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Kilangala ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM ina viongozi bora na shupavu hivyo wasiwe na wasiwasi wajitokeze kwa wingi kupiga kura wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kilangala na kuwataka wazidi kushikamana na CCM kwa maendeleo ya baadae.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli kwa viongozi wa matawi kata ya Kilangala.
 Jiwe la msingi la ofisi ya CCM Tawi la Kilanga
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Mchinga II wakati wa kukagua na kushiriki ujenzi wa zahanati ya Mchinga II
 Wananchi wakisoma vitabu vinavyoelezea utekelezaji wa ilani pamoja na ahadi za CCM  katika kijiji cha Mchinga II vilivyoandaliwa na Mbunge wao Said Mtanda
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Michee ambapo aliwataka wananchi kuweka mkazo kwenye elimu za watoto kwani elimu ndio urithi pekee kutoka kwa mzazi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wakati akiingia kwenye uwanja wa mikutano Milola.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Milola, wilaya ya Lindi Vijijini ambapo aliwaambia
 Umati wa watu ukimsikiliza mbunge wao Said Mtanda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Milola ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Mbunge wa Jimbo la Mchinga Ndugu Said Mtanda akihutubia wakazi wa Milola ambapo aliwaambia asilimia kubwa za ahadi zake zimetimia.
 Wananchi wakiwa mkutanoni Milola.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Milola jimbo la Mchinga ambapo aliwaambia wapinzani wamekosa sera mbadala matokeo yake wamekuwa wakitumia muda mwingi kuishambulia CCM
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ,Mbunge wa Jimbo la Mtama na mlezi wa wilaya Kilwa na Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Bernard Membe akiwasalimia wakazi wa Milola waliojitokeza kwa wingi kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman.
 Msanii wa sanaa ya mashairi  Farida rajabu akiimba utenzi maalum wa mkoa wa Lindi.
 Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye pich ya pamoja baada ya kuwakabidhi vyeti vya kuhitimu mafunzo ya kuendesha boda boda.
Wananchi wa Milola wakiomba kupatiwa kad za uananchama wa CCM kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana

No comments: