Mkuu wa shule ya sekondari ya
Bariadi Bw. Pawa Lutema akipokea msaada wa vitabu vya sayansi kutoka kwa mkuu
wa wilaya Bariadi.
|
Mkuu wa wilaya ya Bariad Bw.
Erasto Sima akisoma Hotuba katika makabidhiano ya msaada wa vitabu vya masomi
ya sayansi kwa shule ya sekondari Bariadi uliotolewa na kampuni ya Airtel
Tanzania.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Shule ya Sekondari Bariadi yanufaika na
msaada huo
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imepiga jeki
jitihada za serikali za kuhamasisha masomo ya sayansi kwa kutoa msaada wa
vitabu vya sayansi kwa shule ya sekondari ya Bariadi iliyopo Mkoani Simiyu.
Msaada huo wenye
thamani ya shilingi milioni 1.5 unahusisha vitabu vya fizikia, hisabati,
baiolojia na kemia kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo shuleni hapo.
Akipokea msaada
huo mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima amesema shule nyingi wilayani
hamo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitabu vya masomo ya
sayansi licha ya kwamba kuna uhaba pia wa walimu wa masomo hayo.
“Ni kweli kwamba
uhaba wa vitabu unakwamisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi kujifunza kwa ufasaha
masomo ya Sayansi wilayani Bariadi hali inayorudisha nyuma ukuaji wa elimu ya
sayansi wilayani hapa”. Alisema Bwana Sima.
“Uhaba wa vitabu
ni moja ya changamoto, lakini uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ni kikwazo
kikubwa kwa utoaji wa elimu ya sayansi kwa wanafunzi wetu hapa Bariadi”
aliongeza Bwana Sima.
Aidha Bw.
Sima ameishukuru kampuni ya simu ya airtel kwa kuona umuhimu wa kuboresha
masomo ya sayansi ambayo ufaulu wake umekuwa mdogo hali ambayo inayotoa
fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa umakini zaidi.
“Msaada
huu utaongeza hamasa kwa wanafunzi wetu kujifunza masomo ya sayansi hivyo
tunawashukuru sana Airtel kwa kuona umuhimu wa kusaidia shule hii na hasa
vitabu vya sayansi” alimalizia Bwana Sima.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya
sekonderi Bariadi Bw. Pawa Lutema akipokea vitabu hivyo, amesema hatua
hiyo ni sehemu ya utatuzi wa changamoto ya vitabu vya sayansi na kisha kuahidi
kuvitunza ili viwe msaada kwa wanafunzi watakaosoma shuleni hapo.
Awali meneja wa Airtel Mkoani
Simiyu Bw. Ezekiel Nungwi akikabidhi msaada huo wa vitabu
amesema kuwa kampuni yake inaendelea na mpango wake wa kutoa msaada wa
vitabu kwenye shule mbalimbali nchini kwa lengo la kusaidia ukuaji wa elimu
nchini.
Msaada huo
wa vitabu vya masomo ya hisabati,kemia,fizikia na Bailojia utasaidia kupunguza
uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye shule hiyo.
No comments:
Post a Comment