Airtel yakabidhi kisima cha maji kwa shule ya msingi Kumbukumbu Dar
· Yaendesha matembezi yahisani kuendelea kuboresha mazingira ya shule.
· Zaidi ya shilingi milioni 10 kukusanywa.
Dar es salaam
Novemba 2014
Kampuni ya Airtel leo imeendesha matembezi ya hisani ili kuchangisha
pesa kwajili ya kuendelea kuboresha shule ya msingi kumbukumbu iliyopo
jijini Dar es salaam
Matembezi
yenye lengo la kupata pesa ili kufanya ukarabati wa darasa la watoto na
kununua viti na meza za kukalia yameetimishwa kwa uzinduzi wa kisima
cha maji kilichojengwa kwa hisani ya Airtel kwa kushirikiana na
wafanyakazi wake ili kukabiliana na tatizo la maji shule hapo
Akiongea
wakati wa kuzindua kisima hicho mgeni rasmi , Kaimu Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,
Benedict Missani kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia na
watoto Mh. Sophia Simba alisema” naunga mkono juhudi zilizofanywa na
Airtel katika kuendelea kuboresha mazingara ya utoaji elimu shuleni
hapa. Nimefurai kuona kuwa Airtel haikuridhika na ujenzi wa kisima hii
tu bali wameamua kuchua hatua nyingine ya kushirikisha wadau mbalimbali
katika kutatua changamoto walizoziona shuleni hapa.
Leo
tumetembe kwa pamoja ili kuweza kuchangisha kiasi cha shilingi milioni
10 zikazowesha kazi ya kuendelea kuboresha mazingara ya shule hii
kuendelea.
Serikali
inaunga mkono dhamira hii na jitihada hizi zinazoenda sambamba na kauli
mbili yetu ya Matokeo makubwa sasa na kuhakikisha tunaboresha maeneo
muhimu hususani elimu kwani vijana hao ndio nguvukazi na taifa la kesho.
Natoa wito kwa mashirika mengine watu binafsi na taasisi mbalimbali
kujitokeza na kuchangia katika shughuli za jamii ili kukubiliana na
changamoto tulizo nazo sasa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema”
nawashukuru wafanyakazi wa Airtel na kila moja aliyeshiriki hapa kwa
kujitoa katika kusaidia jamii, sisi Airtel tumejipanga kutimiza dhamira
yetu ya kuchangia katika kuhakiksha tunachangia katika sekta ya elimu
kwa kuendelea kutoa vitabu na kuboresha mazingira ya shule. Kupitia
mradi wa Airtel Shule yetu tumeweza kuzifika shule nyingi kwa kuwapatia
nyenzo muhimu katika elimu na leo tumewafikia shule ya msingi kumbukumbu
tukiwa na lengo na kuendelea kuboresha sekta ya elimu.
Mpango
huu wa Airtel Tunakujali ni endelevu bado tutakuwa shughuli nyingi
zaidi na shule nyingi zikipokea misaada hivyo tunawaomba wadau
mbalimbali kuendelea kushirikiana nasi.
Kwa
upande wake mfanyakazi wa Airtel Bi Veneranda Boniface Alisema
amejisikia furaha kutumia jumamosi yake kutembea kwaajili yakusaidia
jamii, hii ni sehemu pia ya mazoezi lakini zaidi ni njia pekee ya
kuniwezesha mimi kwa nafasi yangu katika jamii kushiriki kuchangia.
Matembezi
hayo ya hisani yalianzia katika makao makuu ya Airtel yaliyoko Moroco
Dar esaalam na kwenda njia ya Alihasan Mwinyi, kupitia Kaunda, Bongoyo ,
haileselaile , Ali hassani Mwinyi na kuishia katika shule ya msingi
Kumbukumbu.
No comments:
Post a Comment