Tangazo

December 18, 2014

WANAHABARI WASHIRIKI SHINDANO LA KUONJA LADHA ZA BIA ZA TBL ARUSHA

Ofisa wa Kiwanda cha Bia TBL Arusha aliyeo katika idara ya uzalishaji akiwaonyesha baadhi ya wanahabari wa Arusha namna bia inavyohifadhiwa wakati wa ziara ya waandishi iliyokwenda sanjari na zoezi la kuonja bia na kutembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya waandishi wa habari wa Arusha wakiangalia utunzaji wa mazingira unavyofanywa na Kiwanda cha Bia cha Arusha (TBL), ambapo maji yote yanayotumika kwa shughuli za kiwandani hapo huhifadhiwa na kuchunjwa kwa ajili ya matumizi mengine yakiwamo bustani na vyooni, waandishi hao walitembelea kiwandani hapo kwa ajili ya kuongeza ufahamu zaidi wa utunzaji mazingira. 

Meneja Mpishi wa Kiwanda cha Bia TBL Arusha Ben Mwanri akiwasilisha mada kwa wanahabari wa Arusha waliotembelea kiwandani hapo kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali ikiwamo pia zoezi la kuonja Bia lililowashiurikisha waandishi hao wa habari. 

Afisa Uhusiano wa  Kampuni ya Bia nchini (TBL), Edith Mushi akiwapa maelekezo kwa baadhi ya waandishi wa habari wa Arusha waliotembelea kiwandani hapo kwa lengo la kuendelea kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho kilichopo Arusha

: Meneja wa Kiwanda cha Bia Arusha (TBL), Salvatory Rweyemamu akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa zoezi la kuonja bia Deogratisu Moita aliyeibuka mshindi wakati wa zoezi la kuonja bia lilolowashirikisha baadhi ya waandishi wa Arusha, waandishi hao walifanya ziara yao kiwandani hapo hivi karibuni
Afisa wa Usalama Kiwanda cha Bia (TBL) Arusha Heavy Kisena akiwaonyesha baadhi ya waandishi wa habari wa Arusha namna mitambo wa kusafisha maji yanayotoka kiwandani unavyofanya kazi. Waandishi hao walifanya ziara yao hivi karibuni kwa lengo la kujifunza zaidi utunzaji wa mazingira 

Afisa Usalama wa TBL Arusha Heavy Kisena akiwatembeza waandishi wa habari wa Arusha katika maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho wakati wa ziara yao iliyofanyika hivi karibu
Tunaonja Bia: Baadhi ya waandishi wa habari wa Arusha wakishiriki zoezi la kuonja bia lililofanyika kiwandani hapo wakati wa ziara ya wanahabari kiwandani hapo hivi karibuni.

No comments: