Tangazo

December 18, 2014

Aisha Madinda Kuzikwa kesho Ijumaa jijini Dar

Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka (mwenye kilemba cheusi aliyenyanyua mkono), akiongoza kikao cha maandalizi ya mazishi hayo.

- Maziko ya Aisha Madinda sasa yatafanyika Ijumaa tarehe 19-12-2014 mara baada ya sala ya Ijumaa.

- Marehemu Aisha atazikwa Mikwambe Wilaya ya Temeke.

- Msiba upo nyumbani kwao Kigamboni Magogoni jirani na Makaburi ya Wakristo.

- Wadau wanakutana ofisi za Aset leo Alhamisi tarehe 18-12-2014 kwa ajili ya mipango ya mwisho ya maziko.

- Kwa sasa mwili wa Aisha Madinda umeondolewa Hospitali ya Mwananyamala na kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kujua chanzo cha kifo chake.

- Tutazidi kupeana taarifa.
Aisha Mbegu aka Aisha Madinda enzi za uhai wake.

No comments: